steveslove
Senior Member
- Jul 18, 2012
- 110
- 32
- Thread starter
-
- #21
Gap kati ya mtoto wa miaka 7 na miaka 3 ni kubwa sana kwa mtoto. Miaka 7 anajiona ni mkubwa kwa mdogo wake (hata interest zinatofautiana sana) hivyo hawezi kumchangamsha kama ambavyo unadhani anaweza. Kama hamna watoto wengine karibu (3-5yrs) mpeleke day care akachangamshwe na wenzie. Alafu tumia muda mwingi kuongea nae, msemeshe, msikilize na akipatia kitu msifie. Watoto ni wepesi kujifunza haswa anapojua mnamfurahia akijua kitu.
ram sio watoto wote wa kiume wanachelewa bana. Wangu wa miazi 15 ameshajua maneno kibao, mpaka twende nje
(ende nje) anasema. Watoto wanachelewe kutembea/kuongea kwasababu wazazi hawana muda wa kutosha kuwa nao. Ukiwa na muda wa kutosha na mwanao pia usipomlimit (sijui chini ya miezi sita asikae ataumia, kumbeba beba kila saa ndio vitu vinavyolemaza watoto.) mbona atakuwa kama mashine.
mimi ni audiologist, kwa uzoefu wangu mwanao ana speech disoder, angekuwa hasikii na haongei(bubu) ningekushauri ila kwa tatizo la mwanao speech organ zake ni nzito, mpeleke CCBRT Kuna speech therapist watakusaidia kumuintervene, kwani umefanya jambo la maana kudiscaver mapema tatizo la mwanao. wazazi tusifiche ulemauvu wa watoto kwa wao pia wanaweza.
tunakungoja mtoa maada kujua umeshapata ufumbuzi wa mtoto wetu??,kama laa fuata maelekezo niliyokupa hapo juu
hadi miaka miwili kasoro
mimi ni audiologist, kwa uzoefu wangu mwanao ana speech disoder, angekuwa hasikii na haongei(bubu) ningekushauri ila kwa tatizo la mwanao speech organ zake ni nzito, mpeleke ccbrt kuna speech therapist watakusaidia kumuintervene, kwani umefanya jambo la maana kudiscaver mapema tatizo la mwanao. Wazazi tusifiche ulemauvu wa watoto kwa wao pia wanaweza.
kama anatatizo la kusikia na kuongea naweza kukusaidia kumpima na kujua anusikivu kiasi gani na anahitaji tiba gani au msaada gani dadaa.
kaka yake hawezi kuwaza fb he is 7 so bado wanacheza pamoja n they real play all the time, nje anakaa ila haongeagi anacheza bt he doesn't improve
Am very sorry for, pediatrician hana uwezo wa kumsaidia mtoto wako anatakiwa kupelekwe kwa Audiologist wakishirikiana na speech therapist na kufanyiwa speech therapy training. ila bado ni mdogo itaongea tu mkuu.mimi ni me co ke!! Kusikia anasikia vizuri sana hata ukinong'ona na pedetrician alisha mcheki kwenye swala lakusikia
, Ondoa hofu mkuu mtoto wetu ataongea wala usiwe na wasiwasi na mashaka, ila mhimbili sidhani kama kuna audiologist, nilifanya field pale nilimpata mmoja nae alikuwa anafanya research ya masters ujermani. ccbrt ndio nawaamini.nimeenda ccbrt hii huduma kwa sasa haipo aliyekuwepo alishaacha kazi karudi kijijini kwao. Bado nashughulikia appointment ya waliopo muhimbili. So far anazidi kutamka baadhi ya maneno mapya ila huwezi kumwelewa vizuri
Asanteni sana wote mliochangia mada hii kwa sasa mtoto ameanza kuongea na anaongeza baadhi ya vocabularies. Muhimbili wamesema hana tatizo lolote ila chakusikitisha sikupata huduma ya audiologist wala speech therapist. Inasikitisha kuona huduma hizi kwa sasa Tanzania hazipo. CCBRT ilikuwepo hii huduma ila kwa sasa haipo kabisa samilakadunda. Mtoto ameanza shule anaongea anaeleweka tena ngeli kiswahili pia nawashkuru kwa mchango na idea zenu wote