Mwananchi wa Hai auchambua Ubunge Wa Saashisha Mafuwe, ahoji utekelezaji wa Sera ya Kilimo na viwanda.

zanku

Member
Jun 9, 2020
69
149
HAI YA KILIMO NA VIWANDA ALIYOTUAHIDI SAASHISHA MAFUWE IMEANZA KUONEKANA AU NI SIASA ZA MSIMU?

Anaandika Saitabao OleKina, Mkazi wa Kijiji cha Mtakuja


Mwaka 2020 ulikuwa ni mwaka wa kashikashi nyingi, yalitokea matukio mengi mema na mabaya ila Kubwa zaidi wananchi wa Hai tulichagua mbunge mpya baada ya kulizishwa na sera na maono yake juu yetu wananchi.

Mbunge tuliemchagua ni Saashisha Mafuwe baada ya kuinadi manifesto yake namna atakavyofufua uchumi wa kilimo na viwanda uliokufa ndani ya wilaya yetu. Kwa wasiofahamu, sisi wakazi wa hai kwa asilimia kubwa tunaishi kwa kutegemea kilimo na viwanda japokuwa vingi ni vile vidogovidogo. Wengi tulipowasikiliza wagombea ubunge wote kwa maana ya Freeman Mbowe na Saashisha tuliamua kuchagua damu mpya ili tuone ni kwa namna gani ingrweza kutekeleza matamanio yetu baada ya kuchoshwa na siasa za majukwaani zilizojaa malalamiko yasiyokwisha.

Natambua ni mapema sana kuanza kupima utendaji wa Mbunge wetu Saashisha Mafuwe lakini nataka walau nichambue kama zipo dalili za uchumi wa kilimo na viwanda kerejea.

Ni kweli jitihada za huyu kijana damu changa zinaonekana na dhamira yake njema tumeanza kuiona inaenda kutimia, ukiangalia viashiria kadhaa ambavyo ntavitaja hapo chini;

1. MASHINE TOOLS
Tayari mashine mpya na vifaa vipya vimefungwa na kuanza kazi rasmi, hii ni hatua muhimu mno ili kufikia malengo yetu maana kukosekana kwa kiwanda hili ilikuwa ni pigo kwetu walalahoi kwani kiwanda hiki kilikuwa ni kiunganishi na kilikuwa kina-stimulate uchumi wa kila mwana-Hai mmojammoja.

2.MASHAMBA YA VYAMA VYA USHIRIKA
Kwenye hili, hakuna mtu asietambua nikwa namna gani kuyumba kwa mashamba haya kulifanya uchumi ukalala chini, hakuna asiyetambua nikwa kiasi gani watu wa hai wamesomeshwa na mashamba haya wakiwemo kina Marehemu Dkt Mengi, Askofu Shoo na wasomi wengi wa jimbo la hai.

Iko wazi uongozi uliopita ulisababisha mashamba haya yakaporwa na wawekezaji makanjanja ambao waliyakodi mashamba haya kisha wakaua kabisa kilimo na kusababisha baa la njaa na kuanguka kwa uchumi wa mtu mmojammoja ndani ya jimbo letu la hai, si hivyo tu bali wawekezaji hao wababaifu hawakutaka hata kulipa mapato halali ya serikali.

3. MIFEREJI MIKUU YA MAJI

Hali ilikuwa mbaya kiasi kwamba uongozi uliopita ulishindwa kabisa kuchochea wananchi na serikali za mitaa kufanya usafi wa Mara kwa Mara katika vyanzo vya maji na miferejini ili kuhakikisha maji yanapita kwa wingi kuelekea mashambani, tumeona Leo hii Mbunge anashinda mitaani kufanya kazi hiyo ili walau kilimo cha umwagiliaji kiendelee na kuleta ukombozi kwenye uchumi wetu.

4. MIRADI YA MAJI

Mbunge ameonekana Mara kadhaa bungeni akipigania miradi hii ikamilike kwa uharaka, hivi majuzi amefanikiwa kuwasha umeme kwenye mradi kikafu jambo lililokuwa limeshindikana kwa zaidi ya maika 20 ya watangulizi wake. Mradi wa Majimoto Chemka wa visima 20 unaenda kukamilika hivi karibuni kwasababu ya ufuatiliaji wa Mara kwa mara wa mbunge.

5. Mazao ya Mkakati

Wote ni mashuhuda mazao tegemezi kama kahawa yalikosa motisha kabisa lakini chini ya huyu Saashisha tumeanza kuona akiingia vijijini kuhamasisha wakulima warejee shambani na yeye ameanza kusaka makoso ya uhakika duniani kote.
Tumeona amewaleta Tacri, waziri aweso, Pia naambiwa Shirika la redcross limewekeza kwenye mashamba ya ukanda wa tambarare wakifanya kilimo cha mazao ya kimkakati.

Kwa hatua hizi chache nalazimika kukiri na kuamini kuwa Saashisha Elinikyo Mafuwe alikuwa chaguo sahihi la wananchi wa Hai, hii inatoa tafsiri kuwa muda mwingine ni kheri kuweka kando hisia na mahaba ya kisiasa ili kupata maendeleo halisi yanayogusa maisha yetu ya kila siku, can you imagine hata sisi masai wa tambarare tumekumbukwa na Mbunge huyu ilhali kipindi cha nyuma tulisetwa na kutengwa kama wakimbizi.

Wazee wangu wa kimila wameniagiza nimpe jina la "Saashisha Ole Mafuwe" kwa heshima aliyoonesha kwa kabila letu kwa kutuletea barabara ya lami ya dorcas hadi kwenye mapalio yetu ya ng'ombe kule mlima shabaha na sanya station.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom