Wana jamvi tujadili hii Nukuu ndogo tu iliyoandikwa na Mwananchi kuhusu ufisadi TAMISEMI
"
Tumelazimika tena leo katika kipindi kisichozidi wiki mbili kuzungumzia ufisadi unaoendelea kuitafuna Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi). Mwishoni mwa mwezi uliopita, tulichapisha habari za kushtusha kwamba Sh644 milioni kati ya Sh35 bilioni zilizotolewa na wahisani kutoka nchi sita za Magharibi kugharimia awamu ya pili ya Mpango wa Maboresho ya Serikali za Mitaa (LGRP) zimetafunwa na mafisadi wizarani humo.
Tulisema nchi hizo sita za Sweden, Finland, The Netherlands, Ireland, Japan na Ujerumani kwa pamoja zimeitaka rasmi Serikali ya Tanzania kurejesha fedha hizo ambazo zilitumiwa vibaya na mafisadi katika wizara hiyo. Nchi hizo zimesema kila nchi itawasilisha barua ya madai serikalini na kwamba zinasikitishwa na hali hiyo iliyojitokeza kwa sababu kundi linaloumizwa ni la wananchi maskini."
Nchi hii ni yetu sote, namna hii ya ulaji haiwezi kamwe kuleta ustawi wa jamii yetu, watu wachache ambao wamejichukulia madaraka na uhalali wa kutafuna fedha za wananchi pasipo mashaka hawawezi kuvumilika kamwe.
katika mlolongo huu wa ulaji TAMISEMI WAPO wakurugenzi wa halmashauri ambao wamediriki hata kuwahamisha Internal Auditors ambao ni Waaminifu na ambao wamekuwa wakiwabana kwa hoja mbalimbali, wengine hata kufanyiwa timimg na kuibiwa laptop za kazini , na kushtakiwa polisi kwa wizi wa laptop na hatimaye mahakamani. Utashangaa kuona hata taratibu za kiutumishi kuhusu upoteaji wa laptop hazijafatwa wakati hiyo laptop ni less than 1million,wakati pengine Auditor huyu amehoji hoja nyingi kuhusu matumizi mabovu ya mamilioni ya Tsh pasipo action za kueleweka.
Haingii akilini kuona Mkurugenzi anapewa uhamisho, halafu anafanya makeke yake nadani ya miezi miwili tangu kuhamishwa anarudishwa kituo hicho hicho. this is the shame for the Tamisemi!!! Ni wakati wa kuondoa hawa ma internal auditor kuwajibika kwa Wakurugenzi, inabidi wawajibike kwa Chief Internal Auditor au RAS ( ingawa hapa ninawasiwasi pia maana kamfumo haka ka chama hiki cha CCM ni ulaji ulaji tu)
- Mimi nasema ni wakati wa Wabunge wetu tuliowachagua wenyewe pasipo shuruti kwenda mbele zaidi na kuacha ushabiki wa vyama kufanya maamuzi magumu ya hawa MM katika TAMISEMI
- Pili niwakati wa Wananchi wa TZ wapenda maendeleo kuanza kufikiria mfumo mbadala mwaka 2015
Asalaam Aleikum! Bwana Yesu Asifiwe!
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (Laac), imeilipua Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa madai ya kuwa sehemu ya Mtandao wa Ufisadi serikalini.
Tamisemi inaongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia anayesaidiana na manaibu waziri wawili, Aggrey Mwanry na Majaliwa Kassim Majaliwa.
Halikadhalika kamati hiyo ya Bunge imesema, zipo dalili za wazi za kuwapo kwa mtandao wa kutisha wa kifisadi unawashirikisha baadhi ya watendaji wa halmashauri nchini, hazina na Tamisemi.
Tuhuma hizo zilitolewa Bungeni jana na Mwenyekiti wa Laac,Rajab Mbarouk wakati akiwasilisha taarifa ya hoja za kamati kuhusu hesabu zilizokaguliwa kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30,2012.
Alisema bado kuna ubadhirifu,ufisadi na utovu wa nidhamu wa hali ya juu wa matumizi ya fedha za umma kutokana na Tamisemi kutosimamia ama yenyewe kuhusika moja kwa moja na ufisadi huo.
"Mfano mwaka 2011/12, Sh1.6 bilioni zilitumika nje ya bajeti iliyoidhinishwa katika halmashauri 38 na Sh2.6 bilioni zilihamishwa kutoka akaunti moja kwenda nyingine bila kurudishwa,"alisema.
Kamati hiyo imebaini kwamba upo mtindo wa Serikali kutuma kwa halmashauri kiasi kikubwa cha fedha kuliko kiasi cha fedha kilichoidhinishwa na Bunge katika fungu husika wakati wa upitishaji bajeti.
Kamati hiyo imetolea mfano wa Sh2 bilioni zilizotumwa Halmashauri ya Jiji la Tanga na Sh500 milioni zilizotumwa katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe ikiwa ni zaidi ya kiasi kilichoidhinishwa na Bunge.
"Kitendo hiki ambacho kinafanyika kwa ushirikiano wa hali ya juu wa Hazina,Tamisemi na Halmashauri kinaashiria kuwapo mtandao wa kutisha wa kifisadi baina ya mamlaka hizo,"alisema.
Kamati hiyo imeituhumu pia Tamisemi inayoongozwa na Waziri Hawa Ghasia, kuwahamisha haraka watumishi wanaotuhumiwa kufanya ubadhirifu kutoka hamashauri moja kwenda nyingine.
"Kamati imebaini kwamba Tamisemi imekuwa ikitumia mtindo huu kuwalinda watumishi mafisadi ndani ya halmashauri na kuifanya kamati iamini Tamisemi ni sehemu ya mtandao huu,"imesema.
Mwenyekiti wa kamati hiyo alisema kwa makusudi,Tamisemi imekuwa ikieneza saratani hiyo ya ufisadi kwenye halmashauri nyingi iwezekanavyo na kuitaka Serikali kuachana na mtindo huo.
Kamati ya Bunge ya Bajeti, imeishauri Serikali kupunguza matumizi na kuongeza ukusanyaji mapato ili miradi ya maendeleo igharamiwe kwa asilimia 35 ya bajeti ya Serikali.
Akiwasilisha ripoti ya kamati hiyo Bungeni jana, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Andrew Chenge alisema kwa utaratibu wa sasa hakuna uwiano sawia kati ya matumizi ya kawaida na matumizi ya maendeleo.
Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariad Magharibi(CCM) alisema, mwenendo wa deni la taifa si wa kuridhisha kutokana na kuongezeka kwa mikopo ya masharti ya kibiashara na malimbikizo ya riba.