Mwanamziki Tundaman Apata Ajali, anusurika

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Mwanamziki Tundaman apata ajali mbaya Eneo la Idetelo, katikati ya Nyololo na Makambako, aliyekuwa naye katika gari aina ya Toyota Aaron,apoteza maisha. Maiti inapelekwa hospitali ya wilaya ya Mufindi....kwa mujibu wa mpashaji aliyepo Nyololo.

UPDATES

Maelezo ya mwanzo ya Tunda Man amesema ‘Tulikua tunatoka Njombe baada ya kumaliza show yetu na tukasema bora tusilale tuwahi kufika Dar,tumetoka Njombe saa 10 alfajiri mimi nikawa nasikia usingizi nikamwambia mwanangu hebu tuendeshe kidogo,kufika kijiji cha Idetelo kilomita kama 20 au 30 kabla ya kufika Mafinga tukiwa tumelala tukashtuka Gari inaingia porini tukasikia mshindo mkubwa gari imepiga puuuh Dereva hapo hapo akawa amefariki‘

Tunda Man anamalizia kwa kusema ‘Tulikua watu watano kwenye gari aliyekaa mbele na Dereva amevunjika mkono na nyama zimechanika,kuna mtu aliyekua nyuma mapafu yamepasuka,Mimi nipo poa,kwa sasa hivi tuko Mafinga hapa Hospitali ya Wilaya tunaangalia taratibu za kuchukua mwili tuupeleke Kilosa kwa ndugu zake,marehemu aliyefariki anaitwa Mussa lakini watu wengi wanamjua kwa jina la Man katuzo
 

Attachments

  • IMG-20160417-WA0057.jpg
    IMG-20160417-WA0057.jpg
    56.9 KB · Views: 219
  • IMG-20160417-WA0056.jpg
    IMG-20160417-WA0056.jpg
    42.1 KB · Views: 189
  • IMG-20160417-WA0059.jpg
    IMG-20160417-WA0059.jpg
    75.7 KB · Views: 194
Duuh, pole yao... Na hizi mvua ni balaa tupu humu barabarani ..!!

Umesema ni toyota aaron au toyota Aurion ..?!
 
Mwanamziki Tundaman apata ajali mbaya Eneo la Idetelo, katikati ya Nyololo na Makambako, aliyekuwa naye katika gari aina ya Toyota Aaron,apoteza maisha. Maiti inapelekwa hospitali ya wilaya ya Mufindi....kwa mujibu wa mpashaji aliyepo Nyololo.
Auwiiiiiiiiiiiiiiieeeee
 
Mkuu fatilia habari kamili alafu utujuze kwa kina kwa sababu hizi bado ni tetesi ngoja tusubiri habari kamili.
 
Pole sana Tundaman na kwa ndugu wa aliyefariki. Tujitahidi sana kwenda mwendo mzuri na kufuata alama za barabarani
 
Mwanamziki Tundaman apata ajali mbaya Eneo la Idetelo, katikati ya Nyololo la Makambako, aliyekuwa naye katika gari aina ya Toyota Aaron, apoteza maisha.

Maiti inapelekwa hospitali ya wilaya ya Mufindi....kwa mujibu wa mpashaji aliyepo Nyololo.

=====
UPDATE:

Maelezo ya mwanzo ya Tunda Man amesema ‘Tulikua tunatoka Njombe baada ya kumaliza show yetu na tukasema bora tusilale tuwahi kufika Dar,tumetoka Njombe saa 10 alfajiri mimi nikawa nasikia usingizi nikamwambia mwanangu hebu tuendeshe kidogo,kufika kijiji cha Idetelo kilomita kama 20 au 30 kabla ya kufika Mafinga tukiwa tumelala tukashtuka Gari inaingia porini tukasikia mshindo mkubwa gari imepiga puuuh Dereva hapo hapo akawa amefariki

Tunda Man anamalizia kwa kusema ‘Tulikua watu watano kwenye gari aliyekaa mbele na Dereva amevunjika mkono na nyama zimechanika,kuna mtu aliyekua nyuma mapafu yamepasuka,Mimi nipo poa,kwa sasa hivi tuko Mafinga hapa Hospitali ya Wilaya tunaangalia taratibu za kuchukua mwili tuupeleke Kilosa kwa ndugu zake,marehemu aliyefariki anaitwa Mussa lakini watu wengi wanamjua kwa jina la Man katuzo.
 
Hiyo barabara kuanzia mji mdogo wa mafinga mpaka mbeya ni shida. Wakandarasi waongeze tu bidii ikamilike kwa wakati ili ajali zipungue kama sio kuisha kabisa.
 
Back
Top Bottom