SoC03 Mwanamke

SoC03 Mwanamke

Stories of Change - 2023 Competition

Dr leader

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
1,053
Reaction score
1,385
Mwanamke

Sifa yake huruma
Japo kuwa anauma
Mjuvi wa tundama

Kisha anavutia
Machoni ukimtia
Vito utampatia

Ila ana nyuso mbili
Akigeuka tumbili
Usimjue awali

Ana nyingi zake siri
Tena ana umahiri
Hujifanyia kiburi

Pepo kwake rahisi
Atapo ishinda nafsi
Kapambwa na iblisi

Ana mambo na vijambo
Na mwingi wa majigambo
Apendacho ni kugomba

Starehe yangu duniani
Kalisema hilo manani
Na mapambo ya peponi
Na akhera hururaini

Abuuabdillah
 
Upvote 1
Back
Top Bottom