Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Hospitali moja nchini India ambapo mwanamke wa Misri anayeaminika kuwa na uzito mkubwa zaidi inasema mama huyo amepunguza nusu ya uzani wake kutoka kilo zaidi ya 500 hadi kilo 270.
Familia ya Eman Abd El Aty inasema jamaa wao hakuwahi kutoka nyumbani kwa miaka 25.
Bi Abd El Aty alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Saifee miezi miwili iliyopita.
Hospitali hiyo inasema mama huyo anaweza kuketi kwenye kiti cha magurudumu na kukaa chini kwa muda kinyume na hali ya awali.
Bi Abd El Aty alifanyiwa upasuaji unaojulikana kama 'bariatric' na kundi la madaktari wa India wakiongozwa na Daktari Muffazal Lakdawala.
Upasuaji wa 'Bariatric', hufanyika wakati mtu anapokua na unene kupita kiasi na ikiwa hali hiyo inatishia maisha yake.
Dk Lakdawala amesema bi Abd El Aty ameweza kupunguza uzani wake.
Hata hivyo angali anaendelea kupepesuka kutokana na kiharusi alichokipata akiwa ngali mtoto. Pia ana shida ya kuzungumza na ana ugumu wa kumeza chakula.
Hospitali hiyo inasubiri mwanamke huyo kupunguza uzani zaidi ili kuchunguzwa zaidi kuhusu hali ya kiharusi chake.
Dk. Lakdawala, ameongeza madaktari wataanza kumpa mwanamama huyo dawa inayojaribiwa ili kupunguza uzani zaidi. Dawa hiyo imetengenezwa na kampuni ya Marekani.
Familia ya Bi Abd El Aty inasema alizaliwa na uzani wa kilo tano.
Hata hivyo alipokua na miaka 11 uzani wake ulikua umeongezeka, hali ilimsababisha kupata kiharusi na kushindwa kutembea kwa miaka 25. Anatunzwa na mamake na dadake.
Chanzo: BBC Swahili