MWANAMKE SIKILIZA!!!

Sidhani kama hapewi maana kama ni darasa la ndoa wote wanapata, huenda chengamoto ni hapo kwenye kuzingatia.
Sijawahi bahatisha kuona ama kusikia hilo! Ila kama wanapewa kweli inatakiwa msisitizo zaidi! Ndoa za miaka hii ni changamoto mno, sio kwa mwanamke wala mwanaume!
 
Sijawahi bahatisha kuona ama kusikia hilo! Ila kama wanapewa kweli inatakiwa msisitizo zaidi! Ndoa za miaka hii ni changamoto mno, sio kwa mwanamke wala mwanaume!
Maisha ya kuviziana, huenda somo limebadilika siku hizi...badala ya "KAMTUNZE NAE ATAKUTUNZA" imekuwa "KAMUIBIE KABLA HAJAKUACHA UCHUME CHUME"
 
Maisha ya kuviziana, huenda somo limebadilika siku hizi...badala ya "KAMTUNZE NAE ATAKUTUNZA" imekuwa "KAMUIBIE KABLA HAJAKUACHA UCHUME CHUME"
Slogan ni hiyo hiyo "KAMTUNZE NAYE ATAKUTUNZA" ila tu inapotokea unamtunza mtu halafu yeye hakutunzi kwa kweli na wewe moyo wa kuendelea kumtunza unakufa kabisa halafu ukimuuliza kwanini na yeye hakutunzi anakujibu eti ufanye bila kutegemea malipo

Ukiangalia yeye kufanya bila kutegemea malipo hawezi haki ya nani vile wanawake wanaoweza kuishi na wanaume wa aina hiyo nawapa pole kubwa mno mapenzi ni nipe nikupe, toa pokea tofauti na hapo hayo siyo mapenzi ni ufisadi wa kihisia
 
Kwa hilo sawa, na ndio maana ya kukumbushana na kuelimishana.
 
Hahahaa rangi yako halisi..maana hizo sifa hapo juu upo kinyume chake
Hivi wewe unatamani sana kunijua mimi ni mtu wa aina gani eti?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]maana naona unavyohangaika kukisia jinsi nilivyo kutokana na hoja zangu, sasa wacha nikuache uendelee kukisia tu hivyo hivyo na siku nyingine ukikuta nimejibu kwenye uzi mwingine kuwa mimi ni mwanaume napo utaamini tu

Wewe endelea kukariri tu watu kama nyie mnaotaka kujua maisha ya watu msiowajua mitandaoni dawa yenu ni kuwachanganya tu huku naandika hiki kule naandika kile halafu mchague wenyewe muamini kipi muache kipi[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]hii ndiyo jamii forums bwana ukisikia nyingine photocopy
 
Anakusikiliza kwa makini hapo ngoja atoe mkono shavuni sasa!
 
yote nnayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…