Mwanamke raia wa Uganda akamatwa na Passport 15

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,411
Habari wanaJF,

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 40 amekamatwa katika Hoteli ya Lamada akiwa na hati za kusafiria 15 ambapo kati ya hizo 3 ni za Madagascar na 12 ni za Burundi huku akidai kuwa si zake ni za watu walioko Kenya.

Aidha imebainika kuwa lengo kuu ni kusaka visa ya kuwafikisha Saudi Arabia. Kwa mujibu wa Idara ya Uhamiaji Mwanamke huyo atafikishwa Mahakamani siku ya kesho.

Uhamiaji walikuwa wapi siku zote kabla ya Kamishna mpya kuapishwa na kupewa Order ya kubomoa bomoa system yote nahisi wamepanik wanaweza hata jitaja wenyewe kuwa si raia kwa ajili ya wenge...
 
Waliokuwepo uhamiaji watumbuliwe, hii idara limekuwa gang la madarari kwa mda mrefu. Tunaomba watumbuliwe, si vibaya kuanza upya.
 
Duuh nchi imeoza sana hii acha tunanyooshwe, ila katiba na sheria za nchi zifuatwe
 
Uhamiaji walikuwa wapi siku zote kabla ya Kamishna mpya kuapishwa na kupewa Order ya kubomoa bomoa system yote nahisi wamepanik wanaweza hata jitaja wenyewe kuwa si raia kwa ajili ya wenge...

Waliyajua now, kila mtu anataka kukaa kwenye kazi. Mitaani kugumu, bosi huyo lazima atakuwa anashangaa wafanyakazi wake wanavyoleta habari kwake now.
 
Wanajitutumua kujaribu kumridhisha mwana mama Hahahahahaa wa Tz ni actors wazuri Sana Kwa kweli
 
Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 40 amekamatwa katika Hoteli ya Lamada akiwa na hati za kusafiria 15 ambapo kati ya hizo 3 ni za Madagascar na 12 ni za Burundi huku akidai kuwa si zake ni za watu walioko Kenya.

Aidha imebainika kuwa lengo kuu ni kusaka visa ya kuwafikisha Saudi Arabia. Kwa mujibu wa Idara ya Uhamiaji Mwanamke huyo atafikishwa Mahakamani siku ya kesho.

Hili jipu la kusafirisha watu kwenda uarabuni naona halijapata mtumbuaji
 
Mwana mama alisisitiziwa Kuhusu kile Kitengo cha fedha wahasibu jiandaeni kuitwa kwenye interview pale immigration very soon nafasi zitakuwa open
 
Muda Wa watumishi viburi na Miungu Watu wa Immigration kuishi Kama mashetani umekaribia
 
Lamada hotel sio??!!....Moto wa makonda umeanza kujibu..alituambia viunga vya dar vitawaka moto..nimeanza kuamini
 
Habari wanaJF,

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 40 amekamatwa katika Hoteli ya Lamada akiwa na hati za kusafiria 15 ambapo kati ya hizo 3 ni za Madagascar na 12 ni za Burundi huku akidai kuwa si zake ni za watu walioko Kenya.

Aidha imebainika kuwa lengo kuu ni kusaka visa ya kuwafikisha Saudi Arabia. Kwa mujibu wa Idara ya Uhamiaji Mwanamke huyo atafikishwa Mahakamani siku ya kesho.

Safi sana huu mziki usisimame hivyo hivyo mpaka nchi ikae kwenye mstari
 
Back
Top Bottom