Mwanamke nzuri huyu jamanii

Rudi ndani ya mada mkuu
 
Sema, picha nzuri unayodhani ni ya mwanamke. Maana unajuwaje kuwa huyo ni mwanamke?

Mimi naona kama mwanamme aliyewekwa makeup (kachorwa usoni).
 


Wanawake wote ni warembo na hili halipingiki na ndiyo maana usiyempenda wewe yupo mwingine anampenda, ndivyo Mungu alivyoumba.

Lakini urembo kama hidaya kutoka kwa Mungu au kipaji kwa wasanii ni mapenzi ya Mungu, hii haipingiki kwamba wapo wanawake ni warembo kupita wengine, hii ni sawa na mtu anakuwa na akili zaidi ya wengine hatuwezi kusema kwamba wengine hawana akili lakini tunasema mwenzao kawazidi.

Hata kwa wanaume, wapo wanaume jamali (handsome), ukisoma Qur'an (kama hutojali) Nabii Yusufu (as) alikuwa Handsome mithili ya malaika hadi ikatokea kutamaniwa na mke wa waziri, hivyo suala la urembo na ujamali linazidiana kati ya watu na hapa mleta mada nadhani alikuwa na maana hiyo.

Juu ya yote; "ones beuty is in the eyes of the beholder".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…