Mwanamke/msichana anaweza kuamua muda gani wa kupata mchumba?

Blue Bahari

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
1,828
2,153
Wanajamii habari zenu?

Leo nakuja kwenu na mada ya ndoa au uchumba...

Hivi huwa ni kweli mwanamke anaweza kuamua ni muda gani aolewe? Au vile vile kumbe na wao huwa wanatafuta wachumba wa kuolewa nao? (Pale umri wake unaporuhusu).

Ni hivi kuna mabinti watatu tofauti ambao nilimaliza nao shule ya secondary- miaka kumi na mbili sasa. Mpaka sasa niandikapo huu uzi 'ni kwamba hawajaolewa' Nilipowauliza kwanini hawajaolewa mpaka sasa.

Wawili waliniambia "bado hawajaamua tu". Mmoja akanambia yeye bado anatafuta. Lakini vile vile kuna wanawake wawali ambao waliolewa, wakaachika (ni mda mrefu sasa), nilipowauliza (kila mtu kwa wakati wake) kwa nini mpaka sasa hawajapata wenza wengine.Wakaniambia "hawajaamu tu".

Je; ni kweli wanawake/mabinti huwa wanaamua " sasa niolewe au nisiolewe"? Je; ni kweli kwamba na wao huamua aolewe na nani?

Nawaachieni mjadili.
 
Maisha hayana formula kwahiyo usikariri
Wanajamii habari zenu?

Leo nakuja kwenu na mada ya ndoa au uchumba...
Ivi huwa ni kweli mwanamke anaweza kuamua in mda gani aolewe? au vile vile kumbe na wao huwa wanatafuta wachumba wa kuolewa nao? (Pale umri wake unaporuhusu). Ni ivi kuna mabinti watatu tofauti ambao nilimaliza nao shule ya secondary- miaka kumi na mbili sasa.Mpaka sasa niandikapo huu uzi 'ni kwamba hawajaolewa' Nilipowauliza kwa nini hawajaolewa mpaka sasa. Wawili waliniambia "bado hawajaamua tu". Mmoja akanambia yeye bado anatafuta.
Lakini vile vile kuna wanawake wawali ambao waliolewa, wakaachika (ni mda mrefu sasa), nilipowauliza (kila mtu kwa wakati wake) kwa nini mpaka sasa hawajapata wenza wengine.Wakaniambia "hawajaamu tu".

Je; ni kweli wanawake/mabinti huwa uamua " sasa niolewe au nisiolewe"?
Je; ni kweli kwamba na wao huamua aolewe na nani?

Nawaachieni mjadili.
 
''Sijaamua''

Mara nyingi ukisikia ''SIJAAMUA'' ni ufupisho wa sababu nyingi ambazo zipo nje ya uwezo wao, zinaweza kuwa binafsi au si binafsi. Usidanganyike na tabasamu lao usoni, mara nyingi miongoni mwa sababu hizo zaweza kuwa;

  1. Kutokuwa na sifa za kutosha kuolewa/ kuwa wake hivyo kutopata maombi ya uhusiano kabisa
  2. Kupata maombi kutoka kwa watu wasio na sifa ama kuweka vigezo na sifa za watarajiwa zisizo timilika
  3. Uoga wa kuteki risk na utamaduni wa wanawake wengi kuishi maisha ya uongo/kuwa feki.
Mara nyingi sana hata kwetu wanaume, huwa hatuamui kuoa. Tunaoa pale tu tunapopata mtu ambaye tunaamini ''hatuwezi kuishi bila yeye'' ama kwa kuishi naye ubora wa maisha yetu utaongezeka na si vinginevyo. Na ndio maana linapokuja swala la kuoa wote huwa tunamrudia Muumba wetu kwa sala.

Sifa na vigezo vingine hufuata baadaye.

(Ni mtazamo binafsi)
 
Uko deep.
Lakini wakija mabinti, watakubishia
 
Kuamua ni neno tu kama yalivyo maneno mengine. Ila ukweli ni kwamba sisi kama sisi wanawake huwezi kusema utaamua uolewe kesho na ukaolewa hivyo hao uliosoma nao bado hawajawapata wenza wa kusema wawaoe walikujibu hivyo tu kujitia moyo.
 
Kweli. Si limbwata zipo wakiamua kuolewa wanatafuta bwege yoyote na kumtaim tu wakat wa kumpatia(limbwata au mauno) kitu mwaa ndoa inaitika.
We mumy wewee! Mapenzi ya libwata yana athari zake ujue anaweza kupata raha mwanzoni ila mbele ya safari ataona ni bora angebaki single. Na wengine mauno hayawashawishi wanaona kero.
 
waliamua au wanaume ndo adimu kupatikana........?...kuolewa ni bahati vilevile.....so nahisi hawajabahatika.........
 
Kuamua ni neno tu kama yalivyo maneno mengine. Ila ukweli ni kwamba sisi kama sisi wanawake huwezi kusema utaamua uolewe kesho na ukaolewa hivyo hao uliosoma nao bado hawajawapata wenza wa kusema wawaoe walikujibu hivyo tu kujitia moyo.
Vip wewe ushaamua?
 
Back
Top Bottom