Mwanamke kumkubali mwanaume haraka ni dalili ya umalaya?

ila kiukweli wanawake wana changamoto sana kwenye kupata waume. mtu anakutongoza kumbe hujui km ni maskin au tajiri. mtu anaeza kuonekana wa kawaida kumbe ni tajiri balaa afu unamkataa kumbe unakimbia bahati.mwisho wa siku unaangukia kwa mwenzang mimi
 
Mpenzi ni hisia ukiona umetongoza demu anakuzungusha muda mrefu jua hajakupenda na ukilazimisha subiri kuchunwa maana itabidi utumie nguvu ya ziada kumpata, lkn kama amekupenda kutoka moyoni mwake fasta anakukubalia hainaga longo longo
 
Sinaga shida hata akikubali sekunde ya kwanza namtongoza. Ila akinipa na papuchi hapo hapo naona inakuwa kuna shida.
Napenda demu akubali Halafu tuwe na ukaribu usio husisha ku-do kwa muda flani angalau kisha a wiki late or so tuna-do.
 
Niliwahi tongozaga demu nikajitoa mpaka kumfuata kwao huko ndani kijijini na badaboda ya kukodi lakini akawa analeta mashauzi eti ooh unapoteza muda wako mimi nna mtu wangu sijui vikaenda vikarudi nikarudi tena mara ya pili lakini waapi nika msajilia laini special kwa ajili yake na nikaijaza bando la mwezi mzima in case anapata maamuzi anijulishe lakini waapi mara ya tatu nikaenda tena kijijini kwao na kumwimbisha tena lakini waapi nilichoamua siku hiyo ni kumwambia kwaheri na nakutakia kila la kheri , hakuona unyayo wangu mpaka leo baadae akawa ananitafuta kwenye simu huku akiona aibu hata kuhitambulisha lakini nilikuwa nazijua namba anazozitumia kwa hakika upendo ulitumbukia nyongo na leo hii nna binti mrembo sina stress ile imebaki story
 
Back
Top Bottom