Mwanamke kudai haki sawa ni kiburi, mwanaume kudai haki sawa ni aibu

GREENER

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
641
2,131
Habari zenu wanajamvi, poleni kwa pirika za hapa na pale za kuumalizia mwaka 2016; kama ilivyo kawaida katika maisha ya mwanadamu wapo wanaoumaliza kwa huzuni na wengine kwa furaha, mwisho wa siku tumshukuru Mungu kwa kila jambo.

Kabla ya kuumaliza mwaka huu, niliona vyema kufanya tathmini ya mada au nyuzi zetu nyingi katika jukwaa letu hili pendwa.

Nimeona nyuzi nyingi humu wanawake wakiwashutumu wanaume na wanaume wakiwashutumu wanawake kuhusiana na usawa katika Nyanja mbalimbali na kila mmoja alitoa sababu zake na wapo waliotoa sababu zenye mashiko hasa.

Leo nami napenda nitoe mtazamo wangu (sio sharia, its just a mere opinion) kuhusiana na swala Zima la usawa kati ya mwanamke na mwanaume katika mapenzi.

Mwanamke kudai usawa kwa mwanaume ni kiburi

Hapa naomba kwanza niweke wazi kua nazungumzia usawa kwa wanandoa au watu walio kwenye mahusioano sio ule wa katika jamii generally coz huo nao ni mjadala wenye upana wake.

Wanawake wengi tunapenda kua treated sawa na vile sisi tunavyowatreat wanaume zetu, yani tunapenda titi fo tati, kila anachofanya mwanaume na sisi tufanye na wakitukataza tunawauliza mbona wewe unafanya? My dear lady, we should know our position, tangu kuumbwa kwa ulimwengu (nazungumzia kwa imani yangu ya kikatoliki), mwanaume kaumbwa kua kichwa kwa mwanamke, mwanamke umetokana na ubavu wa mwanaume there is no way sisi viumbe viwili tukawa sawa, kwenye maisha lazima kuwe na kiongozi na muongozwa, asili ya mwanaume ni kumuongoza mwanamke na kumlinda, hivyo nasi tukubali asili yetu ya kuongozwa na kulindwa nao ili maisha yaende, tunapokataa ukweli huu ndo tatizo linapoanza. But kuna aina za uongozi ambazo hata Mungu hapendi hivyo hapa namaanisha wanaume hampaswi kutumia asili yenu kuwanyanyasa wanawake bali muwaongoze kwa haki yani you have to step on her shoes ( jiulize; je mimi ningekua mwanamke ninge ongozwa kwa staili hii nnayomwongoza ningejisikiaje?).Biblia inasema " enyi wanawake watiini waume zenu na enyi wanaume wapendeni wake zenu", ukitafakari hilo neno utaona kabisa kua mwanamke anahitaji kumtii mwanaume coz mwanaume ni kiongozi, na mwanaume anahitaji kumpenda mwanamke coz mwanamke ni kiumbe dhaifu kwa mwanaume ( udhaifu wa hapa sio wa maana mbaya) hivyo kinahitaji upendo kutoka kwa kiongozi wake.

Hebu assume mazingira ambayo mwanamke anamtii mwanaume coz anaamini ni kichwa cha mahusiano na mwanaume anampenda mwanamke coz anaamini ni kiumbe kilicho chini yake yake hivyo yeye yuko responsible for her in every aspect; mahusiano lazima yadumu.

Usiombe huyo mwanaume siku akakutana na mwanamke aliyefunzwa kumtii na kumheshimu mume, utabakiwa na manyoya tu.

Wanawake tusidanganywe na hizi NGO za kupigania haki sawa kwanza ukichunguza wanaharakati wao wengi hawajaolewa au wamebaki na ndoa jina, coz kwenye maisha ya ndoa hakuna haki sawa sawa kati ya mke na mume, dai upendo kutoka kwa mumeo hilo ndo jukumu lake alilopewa na Mungu kwako sio kudai haki, Upendo ndo kila kitu


Mwanaume kudai haki sawa ni aibu

Hili tatizo linakua kwa kasi sana miaka hii ya karibuni na litaendele kukua kutokana na maisha kua magumu na wanaume kutoheshimu nafasi au hadhi zao.

Unakuta mwanaume yupo kwenye ndoa au mahusiano halafu anadai haki sawa za kimajukumu kutoka kwa mke au gf wake hii ni aibu hasa kwa mila za kiafrika.

Mwanaume wewe ni kichwa cha familia na unafurahia ukisikia unaambiwa wewe ni kichwa but kwanini hutaki kubeba majukumu ya huo ukichwa? Tangu kuumbwa kwa ulimwengu mwanaume kaambiwa atakula kwa jasho, maana yake; kwakua yeye ni kichwa jasho lazima limtoke kwajili ya viuongo vyote vinavyoshikilia kichwa (supportive organs), na alipewa mwanamke kama msaidizi so yeye kama master wa huyo msaidizi he is full responsible for her.

But siku hizi ni jambo la kawaida kwa mwanaume kudai haki ya usawa wa mgawanyo wa majukumu ya kulisha/kutunza familia, my dear gentleman you should know your place. Wewe kama mwanaume inabidi uwajibike kwa asilimia mia moja kwa familia yako, kama mwanamke pia anakipato usimlazimishe atoe muache atoe pale anapoguswa yani kipato cha mke wako kiwe kama nyongeza tu au bonus kwako na sio umpangie sharia hyo ni aibu na ndio mwanzo wa baadhi ya wanawake kuwadharau waume zao coz wanakwepa majukumu hivyo mwanamke anajikuta anaplay role zote mbili ya ubaba na mama so anaona hampo tofauti na dharau zinaanza.

kama matumizi yenu ya mwezi ni milioni ( kodi ya nyumba, nauli, chakula, pocket money ya watoto,dharura, mavazi, n.k) hakikisha unafight kupata hyo milioni kila mwezi hata kama mkeo anakipato kikubwa, hyo itakupa heshima kwa mkeo na lazima akupe support na hata kama utaikosa hyo pesa mkeo atatoa pesa kwa moyo wote coz anajua mme wake ni mtafutaji but this time kakosa. Kuliko ukidai usawa katika jambo hili hata siku ukikosa mkeo atajua ni uzembe wako au kusudi coz umejua yeye anapesa.

Na hata kama kipato chako hakikidhi mahitaj ya familia kutokana na ugumu wa maisha tafuta njia ya kufikisha ujumbe kwa mkeo ili msaidiane na sio kudai usawa na kumlazimisha yeye aone hilo ni jukumu lake, hiyo ni aibu kubwa na inakushushia heshima.

Usiombe siku mwanamke wako akakutana na mwanaume anayejua kula kwa jasho, maji utaita mma

Hitimisho.

Penye pendo la dhati kila mmoja ataona furaha na fahari kutimiza wajibu wake , hatochukulia wajibu kama adhabu, UPENDO ndo nguzo ya maisha ya mwanadamu, kabla hujamlaumu mwenza wako jiulize 'je mimi nimetimiza wajibu wangu ipaswavyo?' isijekua kutotimiza wajibu wako ndiko kuliko pelekea mwenzi wako kufanya hayo anayo yafanya.
 
KAMA MTU ATADAI HAKI SAWA, KWA MAANA YA HAKI ZA BINADAMU, NI SAHIHI.

ILA KAMA ATADAI HAKI SAWA , KWA MAANA YA KUGAWANA MAJUKUMU YA KIJINSIA HUO NI UJINGA.

MWANAMKE ATAENDELEA KUWA MWANAMKE, NA MWANAUME ATAENDELEA KUWA MWANAUME.

MAMBO YAKIENDELEA HIVI MWISHO WA SIKU MWANAMKE ATAOMBA ASAIDIWE KUBEBA MIMBA.
 
KAMA MTU ATADAI HAKI SAWA, KWA MAANA YA HAKI ZA BINADAMU, NI SAHIHI.

ILA KAMA ATADAI HAKI SAWA , KWA MAANA YA KUGAWANA MAJUKUMU YA KIJINSIA HUO NI UJINGA.

MWANAMKE ATAENDELEA KUWA MWANAMKE, NA MWANAUME ATAENDELEA KUWA MWANAUME.

MAMBO YAKIENDELEA HIVI MWISHO WA SIKU MWANAMKE ATAOMBA ASAIDIWE KUBEBA MIMBA.
Yap mwanamke ataendelea kuwa mwanamke period....
 
wote wanaodai vilivyozuwiliwa na Mungu (ambavyo havikupangwa)
wana hatia, dunia haiwezi kuwahurumia wala Mungu hawezi kuwavumilia, wasubiri majanga tu
 
Kwa wale wanaume vidume tunashika nanii zetu na kwa sauti tuseme wanaume hoyeee
 
Back
Top Bottom