Mwanamke jela kwa kufanya mapenzi na mtoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke jela kwa kufanya mapenzi na mtoto

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MaxShimba, Mar 25, 2010.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Daniel Mjema, Moshi

  Gazeti la Mwananchi

  MWANAMKE ambaye ni mke wa mtu mwenye watoto watatu, amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mapenzi na mwanafunzi wa kidato cha kwanza mwenye umri wa miaka 15.


  Mbali na mwanamke huyo, Sophia Philemon (44) mkazi wa kambi namba tisa katika kiwanda cha sukari cha TPC, wilaya ya Moshi vijijini kuhukumiwa kifungo hicho, pia ameamriwa kumlipa mwanafunzi huyo fidia ya Sh1 milioni.


  Hukumu hiyo, ilitolewa jana mjini Moshi na Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa Kilimanjaro, John Nkwabi baada ya kuridhika na ushahidi wa mashahidi wanne wa upande wa mashitaka.


  Nkwabi alisema ushahidi wa mashahidi hao, akiwemo mwanafunzi huyo wa sekondari ya Langasani, umeithibitishia mahakama pasipo shaka yoyote kwamba mwanamke huyo, alimlazimisha mtoto huyo kufanya naye tendo la ndoa.

  Kitendo hicho ni kosa chini ya kifungu namba 138B (1) (d) cha kanuni ya adhabu kinachosimamia makosa ya kimapenzi kwa watoto baada ya sheria hiyo kufanyiwa marekebisho mwaka 2002.


  Hakimu Nkwabi alisema mahakama imeridhika na ushahidi kuwa Februari 28, mwaka jana, saa 1:00 usiku huko kambi namba tisa, mshitakiwa alimlazimisha mwanafunzi huyo kufanya naye mapenzi katika chumba anachoishi na mumewe.

  Muda huo, mwanafunzi huyo alikuwa ametoka dukani alikokuwa ametumwa na wazazi wake na mwanamke huyo, alimwita na kumshawishi aingie ndani ya nyumba yake na baadaye kumlazimisha kufanya naye tendo la ndoa.


  Baada ya kutiwa hatiani, wakili wa serikali, Hellen Moshi aliyeendesha kesi hiyo, aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwani vitendo vya ubakaji vinazidi kuongezeka nchini hususan kwa watoto wadogo na wanafunzi.


  Katika utetezi wake, Sophia alisema ni mke wa mtu na hakubahatika kupata mtoto na mwanaume huyo, lakini kabla kuolewa alikuwa tayari amezaa watoto watatu, wawili wa kike na mmoja wa kiume.

  Mshitakiwa alikuwa alikataa kufanya tendo la ndoa na mtoto huyo, licha ya kumfahamu kuwa ni jirani yake. Utetezi wake ulitupiliwa mbali na mahakama hiyo.
   
 2. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  mhhh kazi ipo mama mzima kumvulia chupi mtoto....
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  miaka 15 sio mtoto.....
  we jaribu kumvulia mmoja uone kazi yake....
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,335
  Likes Received: 22,187
  Trophy Points: 280
  Hii ilikuwepo juzi hapa na tukachangia sana..
  Naona umeileta kwa mara ya pili.
   
 5. Abraham

  Abraham Senior Member

  #5
  Mar 26, 2010
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 115
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Naomba kujua... mbona naona kama hiyo adhabu ni ndogo sana . Mi nilifikiri makosa ya kubaka adhabu yake ni 30 yrs +... au inategemea aliyebakwa ni wa jinsia ya kiume au ya kike? Naomba mwongozo
   
 6. Mapondela

  Mapondela JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa bahati mbaya sheria yetu ya makosa ya kujamiana tendo la kubaka limeelemea kwa wanaume tu ndio wanaweza kubaka mwanamke anabaka pale anapomsaidia mwanaume kubaka, kitu ambacho kwa hili naona ni changamoto katika sheria hii.

  Huyu bi mkubwa pepo wake mbaya. Angekuwa hana mume tungesema uzalendo ulimshinda lakini ..................Mmmmmmmmm
   
 7. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Nina mashaka, kama huyu mtoto hakukubaliana na huyu mama kwa nini hakupiga kelele majirani waje? Au pengine alimwahidi kuwa baada ya tendo hili atampa hela na hakumpa hivyo mtoto akaamua kuifanya issue. Hakuna mtu anaweza kumlazimisha mwanaume kwa tendo lile!!!
   
 8. gwambala

  gwambala Member

  #8
  Mar 26, 2010
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mmh mi nahisi kijana naye aliipenda sema madingi zake ndo wakawa wakali
   
 9. T

  Tall JF-Expert Member

  #9
  Mar 26, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  kweli ni mtu mnzima huyo.
   
 10. Z

  Zamazamani JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2010
  Joined: Jun 13, 2008
  Messages: 1,624
  Likes Received: 339
  Trophy Points: 180
  Dogo alikuwa anapata raha...hawa vipi?angekuwa hataki mashine ingesimamaje? tena na kucheua....wamwache mama ili dogo aendelee kufaidi
   
Loading...