Polisi Moshi katika kashfa ya ujambazi Send to a friend Sunday, 19 December 2010 20:25 0diggsdigg
Daniel Mjema, Moshi
POLISI wa kikosi cha pikipiki mkoani Kilimanjaro ni mshiriki mkuu wa tukio ambalo mtunza fedha wa kampuni ya Machare Investment ya mjini Moshi aliporwa Sh7.5 nje ya Benki ya NBC tawi la Moshi, ilidaiwa mjini hapa.
Habari zilizopatikana jana, zilipasha kuwa pikipiki mpya ambayo haijasajiliwa iliyotumika katika tukio hilo iliazimwa na polisi mmoja kutoka kwa mfanyabiashara (jina tunalo) ambaye naye anashikiliwa na polisi.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo vya habari,katika tukio hilo polisi huyo ndiye anayedaiwa kutoa laini kwamba mtunza fedha huyo angepeleka benki kiasi kikubwa cha pesa juzi ambapo polisi alikuwa apate mgawo wa Sh15 milioni.
Hata hivyo kiasi alichokuwa nacho mtunza fedha huyo, Caroline Ibrahim kilikuwa ni Sh 7.5 milioni tu na kilifanikiwa kuokolewa baada ya mwanamke huyo kumngangania kiunoni mmoja wa majambazi huyo aliyekuwa na pikipiki.
Habari hizo zilidai polisi huyo alikuwa mmoja wa askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wanaolinda benki hiyo kabla ya kuhamishiwa kikosi cha pikipiki kilichoasisiwa na KamandaVenance Tossi aliyewahi kuwa RPC Kilimanjaro.
Inadaiwa kuwa polisi huyo alikuwepo eneo la tukio lililotokea juzi saa 5:00 asubuhi. lakini alifanikiwa kutoroka alipoona mshirika mwenzake amenganganiwa na mtunza fedha huyo huku akipiga kelele za kuomba msaada.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, baada ya kushindwa kwa mpango huo wa uporaji na polisi huyo kukamatwa, alijitetea kuwa pikipiki hiyo iliibwa muda mfupi tu baada ya kuazima, lakini hakuwa ameripoti tukio hilo kituo chochote cha polisi.
Habari za uhakika ambazo Mwananchi inazo, zinadai polisi huyo anashikiliwa kituo cha Himo huku kijana aliyekamatwa red hended akihifadhiwa kituo cha Polisi Bomangombe na mfanyabiashara akiwa polisi Majengo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Nghoboko alisema jana kuwa uchunguzi wa awali wa polisi unaonyesha kuwepo kwa ushiriki wa polisi mmoja katika tukio hilo ingawa alikataa kumtaja kwa jina.
Inaelekea kuna polisi wetu mmoja ameshiriki katika tukio hili ambalo kwa kweli limetufadhaisha sana, lakini naandaa taarifa rasmi hapa nitaitoa kwa waandishi wa habari kesho (leo),alisema Kamanda Nghoboko alipohojiwa jana.
Tukio hilo ambalo limekuwa gumzo mjini hapa, lilitokea nje ya Benki ya NBC tawi la Moshi juzi saa 5:00 asubuhi na mwanamke huyo anachukuliwa kama ni mwanamke jasiri aliyapambana na kufanikiwa kuokoa fedha zilizoporwa.
Katika purukushani hizo, wananchi wakiwemo madereva wa taxi walijitokeza kumsaidia mwanamke huyo ambapo jambazi huyo alipatiwa kibano cha nguvu kabla ya polisi kufika eneo hilo na kumtia mbaroni akiwa hoi bin taabani.