Mwanamke hupevuka kiakili mapema kuliko mwanaume

Mwanamke hupevuka kiakili mapema kuliko mwanaume

Daudi1

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2013
Posts
15,840
Reaction score
26,250
Habari ya asubuhi wanajamii ya humu kwetu,kama ilivyo desturi yetu kushirikishana ili kudumisha mahusiano yetu karibu ushiriki mawazo yako ni ya msingi sana
Nanukuu......................

"Imekuwa ni dhana ya muda mrefu miongoni mwa wanajamii katika Afrika kuwa msichana hawezi kuolewa na mwanamume waliyelingana umri kwa kuwa ni vigumu kuelewana na kuheshimiana.

Dhana hiyo inajikita katika kuchambua tofauti ya ufahamu kati ya mwanamke na mwanamume wenye umri sawa. Mwanamke huwa na akili iliyokomaa zaidi kuliko mwanamume wa umri huo huo. Utafiti mpya umeipa uzito nadharia yao, baada ya kugundua kuwa ubongo wa msichana hukomaa haraka kuliko wa mvulana.

Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Newcastle wamasema hii inaweza kusaidia kuelezea sababu za wasichana wadogo kuonekana kukua kwa kasi zaidi, kuliko wenzao wa kiume wenye umri sawa.

Wanasayansi walitumia kipimo maalumu kwa ajili ya kuchunguza ubongo kwa watu 121 waliokuwa na umri kuanzia miaka minne hadi 40. Matokeo ya utafiti huu yalionyesha kwamba mchakato wa kubalehe huanza kati ya miaka 10 kwa msichana, huku mvulana huchukua muda mrefu kuanzia miaka 11 mpaka 20.

Dk. Marcus Kaiser, ambaye nbi mtafiti, anasema: "Hii ni sehemu ya mchakato wa kawaida wa kujifunza ubongo kwa jumla.

"Kwa kawaida hata katika utambuzi, imeonekana kwamba msichana ana uwezo wa kushika mambo mengi zaidi kuliko mvulana, ndiyo maana katika nchi za Afrika mtoto wa kike anapika, anajaribu kutekeleza majukumu ya nyumbani kama mama yake, bado shuleni atafanya vizuri, lakini si kwa mvulana. Akishazongwa na mambo mengi hupunguza morali shuleni."

Dk. Kaiser anafafanua kuwa hatua za ukuaji wa mtoto wa kike ni za haraka ukilinganisha na wa kiume. Hii inatokana na mfumo wa kike. Binti hukua haraka kutokana na homoni zake mwilini na pia akishabalehe ndipo anakuwa na uelewa mpana kutokana na via vyake vya mwili kumruhusu kubeba ujauzito."

Wataalamu nchini

Tuzie Edwin, ambaye ni msemaji wa Afya ya Mama na Mtoto kutoka Kituo cha Huduma ya Ushauri Nasaha, Lishe na Afya (COUNSENUTH), anasema mtoto wa kike huanza kupevuka kiakili ndani ya miezi mitatu baada ya kuzaliwa.

"Ukuaji wa ubongo wa mtoto wa kiume na wa kike ni tofauti sana. Akili ya Msichana huanza kukua kumzidi wa mvulana ndani ya miezi mitatu ya mwanzo tangu kuzaliwa. Katika uchunguzi wa wazazi watagundua kwamba wakati wanapomlea mtoto wa kike, huongea haraka zaidi kuliko wakati wa kulea mtoto wa kiume," anasema Tuzie na kuongeza:

"Msichana hutambaa na kutembea haraka zaidi ukilinganisha na mvulana, hata katika kuongea. Pia huwa na uelewa mpana wa mazingira, anakuwa mwepesi kuanza kutumia choo mapema na ana kumbukumbu kwamba hivi sasa anahitaji kujisaidia na pia huanza kujitegemea ndani ya miaka miwili ikilinganisha na wa kiume," anasema Edwin.

Anasema msichana huwa mwepesi katika kuwasiliana na pia huweza kuanza kushirikishwa katika baadhi ya mambo, kama kutumwa dukani mapema zaidi ukilinganisha na mvulana.

"Msichana pia anawahi kupevuka ukilinganisha na mvulana, lakini akishabalehe tu ubongo wake hukomaa haraka na hapo ndipo maumbile yake yanapoanza kujitengeneza mapema kwa ajili ya mwili kujitayarisha kubeba ujauzito wakati wowote. Hata hivyo akili yake hukua kwa nafasi kubwa kipindi hiki, ukilinganisha na mwanamume ambaye ni hadi miaka 10 baadaye," anasema Edwin.

Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi katika Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Dk. Elifatio Towo anasema mtoto yeyote ana uwezo wa kukua kwa haraka zaidi, kutokana na namna mzazi anavyomlisha na haina tofauti na jinsi yake.

"Ikumbukwe kwamba mtoto yeyote anaweza kukua kwa haraka zaidi ikiwa mzazi atampa lishe bora na matunzo mazuri.

Kunyonyesha ndiyo sababu pekee inayowafanya watoto akili zao zikue kwa haraka zaidi. Lakini ikumbukwe kwamba watoto wa kike huwa na busara zaidi katika baadhi ya mambo na katika kufanya uamuzi ikilinganishwa na wa kiume," anasema na kuongeza:

"Huyu anaweza kufikiria makubwa zaidi ya umri alionao, lakini mara nyingi inatokana na maumbile kwamba yeye ni mwanamke hivyo kupevuka na anakuwa tayari kubeba ujauzito, mwili wake unajitengeneza wenyewe," anasema Dk. Towo." Mwisho wa kunukuu chanzo mwananchi........................

My take watu wamekuwa wakisema katika mahusiano umri hauna tatzo,kwa ninavyojua hakuna mwanaume anayependa kuwa chini ya mwanamke hata wanawake huwa wanajisikia raha wanapokuwa na mahusiano na mwanaume aliyewazidi nyie hili mnalionaje? ni kweli katka mahusiano umri hauna athari yoyote? tutafakari pamoja weekend njema
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
​
 
Mtoto wa kike anakomazwa na majukumu toka utotoni, fanya utafiti katika familia mbali mbali zilizoko mijini humu na zile za vijijini.....

Kuna kitu kikubwa sana kinawatenganisha na kuwatofautisha watoto wa kike/wanawake katika mazingira niliyosema..
 
Yani very true,No wonder vijana agemates hawanivutiii...yn akili zao zinawaza bata tu,sio maendeleo...
Mwanaume akikuzidi ina raha yake coz ana uelewa wa maisha (maturity) and u can look up to him..
 
Yani very true,No wonder vijana agemates hawanivutiii...yn akili zao zinawaza bata tu,sio maendeleo...
Mwanaume akikuzidi ina raha yake coz ana uelewa wa maisha (maturity) and u can look up to him..
Kuna watu wasema umri ni namba tu hilo kwa upande wako unalizungumziaje?
 
Mtoto wa kike anakomazwa na majukumu toka utotoni, fanya utafiti katika familia mbali mbali zilizoko mijini humu na zile za vijijini.....

Kuna kitu kikubwa sana kinawatenganisha na kuwatofautisha watoto wa kike/wanawake katika mazingira niliyosema..
Ni kweli mkuu hapo unatofautisha kati ya wale waliokulia mijini na vijijini,unaongeleaje suala la mahusiano kati ya mwanaume na mwanamke ambao wako sawa au mwanamke amemzidi mwanaume je umri una athari?
 
Kwangu haimati as long as wote akili zenu zimekomaa na mnauwezo wa kupambanua mambo na mnamawasiliano mazuri
 
Ni kweli jiulize tu wasichana wale ambao umewaacha darasa la saba(hawakupata fursa ya kuendelea) ukasoma hadi chuo ukirudi mtaani wana watoto ambao wako dARASA LA TATU yaani wanakomazwa na majukumu. wanawake..........ikipita miaka 5 later hujaoa unaweza kibazazi bazazi ukammendea mtoto wa classmate wako anakua tayari yuko mature
 
Kuna watu wasema umri ni namba tu hilo kwa upande wako unalizungumziaje?

hyo concept ya umri kuwa namba naona ina work out mwanaume akishakuwa mtu mzima walau na akili timamu za kimaisha...mfano binti 25 yrs datinga 20 yr old boy NI UTATA MTUPU,hakuna kitu hapo...but mwanamke lets say 35 yrs dating a 30 yr old man inawork being a cougar cz mwanaume kashakua huyo,,japo i alii 2 cases mwanamke kazidi 5 yrs..
 
Ni kweli jiulize tu wasichana wale ambao umewaacha darasa la saba(hawakupata fursa ya kuendelea) ukasoma hadi chuo ukirudi mtaani wana watoto ambao wako dARASA LA TATU yaani wanakomazwa na majukumu. wanawake..........ikipita miaka 5 later hujaoa unaweza kibazazi bazazi ukammendea mtoto wa classmate wako anakua tayari yuko mature
Hahahahaaaaa umenichekesha mkuu
 
Kwangu haimati as long as wote akili zenu zimekomaa na mnauwezo wa kupambanua mambo na mnamawasiliano mazuri
Kwako umri hauna tatzo? wanawake huwa wanamfanya mwanaume kama mlinzi wake kwa kila jambo je inakuwaje uauwa na mlinzi uliyemzidi umri huoni kujiamini kunapungua?
 
Kwako umri hauna tatzo? wanawake huwa wanamfanya mwanaume kama mlinzi wake kwa kila jambo je inakuwaje uauwa na mlinzi uliyemzidi umri huoni kujiamini kunapungua?

Kutapungua kama huyo nwanaume ana akili za kitoto ila kama kakomaa kiakili bado anaweza kuwa mlinzi kama anajiamini
 
my proffesor used to say mrn never grow beyond the age of five...mentally
 
Ki science ni kweli. umri ukipishana hata heshima inakuwepo hasabaada ya miaka 5 na kuendelea ya ndoa
 
Hii mada umeitoa kwenye gazeti la mwananchi, yah ni kweli nime experience hich kitu
 
Back
Top Bottom