IKARAHANSI
JF-Expert Member
- Jul 30, 2019
- 398
- 479
Baadhi ya wanaume hasa vijana wanapovunja mahusiano na wasichana/wapenzi wao huanza kuwatolea siri za ndani hasa maungoni na kuzitangaza hazarani kwa kudhani kuwa wakifanya hivyo watakuwa wanawakomoa na wanawake/wasichana hao hawatapata wapenzi wengine.
Mfano waweza kukuta kijana wa kiume akimtangaza msichana walieachana naye kuwa ana "bwawa", (binafsi naona huku ni kujidhalilisha). Lakini jambo tunalopaswa kujua ni kuwa ukimtangaza msichana kuwa ana "bwawa" lazima ujue kuwa Wakulima wa mikoani watakuja kufanya utafiti kuona kama linafaa kwa kilimo cha umwagiliaji, sasa kabla ya utafiti lazima watalipia ada na kawaida ada huwa hairudi iwe umefanikiwa ama la.
TANESCO wakisikia "bwawa" lazima walitafute ili kuona kama linaweza kuzalisha umeme wa kuingiza kwenye grid ya taifa ili kuwezesha uzalishaji wa umeme utakaoliwezesha taifa kwenda kwenye uchumi wa kati, nao watakuja na kulipa ada (fedha) ili kufanya utafiti kuona kama wanaweza kupata umeme. Ada hiyo haitarudishwa (bila kujali kama wamefanikiwa ama hawakufanikiwa)
TBS hawa ni shirikika la taifa la kudhibiti viwango na ubora wa bidhaa, wao wakisikia" bwawa" wanakuja kuangalia ubora na pia kulithibitisha (kuna watu hawajui kutofautisha kati ya bwawa na dimbwi) kabla ya kufanya kazi hiyo watalipa "ada" (ambayo haitarudishwa) lengo la utafiti wa TBS ni kuona na kutambua kama ni bwawa kweli au ni dimbwi ili waweze kupeleka taarifa sahihi serikalini na kuiwezesha kuandaa mpango kazi kulingana na hali ya eneo husika
Je! Mwanamke/Msichana mwenye hilo "bwawa" ambaye ulimtangaza ili kumkomoa na sasa amepokea "ada" zote hizo unadhani anaweza kuwa mwenzako kiuchumi? baadae utakuja tambua kwamba ulimpiga chura teke na hivyo kumuongezea mwendo
WANAUME WENYE TABIA YA KUTANGAZA MADHAIFU YA WAPENZI WETU TUJITATHIMINI UPYA MAANA MWANAMKE HAKOMOLEWI.
Uzi tayari karibuni kwa michango na maoni pia ushauri bila kusahau mapovu!!