Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,563
- 21,665
Watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamemuua kwa kumpiga risasi mkazi wa mtaa wa Ibungilo, kata ya Nyamanoro wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza Monica John na kuwajeruhi watu watatu ambao wamelazwa katika hospitali ya rufaa Bugando na kisha kupora kiasi cha fedha ambacho hakijajulikana.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Zarau Mpangule, amesema tukio hilo limetokea aprili 27 majira ya saa 1.45 usiku baada ya majambazi hao waliokuwa na silaha inayoaminika kuwa ni SMG kuvamia duka la m –pesa, tigo – pesa na airtel money mali ya Thomas Oganga na kumuua mke wake kwa kumpiga risasi kichwani na kisha kutokomea kusikojulikana.
Kaimu Kamanda huyo wa Polisi mkoani Mwanza SSP Mpangule, licha ya kueleza kuwa jeshi la Polisi mkoani humo limeanza msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa wa mauaji hayo ili kuhakikisha wanakamatwa na hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi yao.
Maganda matatu ya risasi yameonekana katika eneo la tukio, huku baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo, akiwemo binti mmoja ambaye ni mkazi wa Kiseke aliyekuwa akisaidiana na marehemu Monica John kufanya biashara ya pesa katika duka hilo wakisimulia hali ilivyokuwa.