real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,302
Ni baada ya kuchinjwa kasha kucharangwa na mapanga.
Mwanamke mmoja ambaye ni mkazi wa Kijiji cha China Kata ya Kate, Nkasi, Rukwa, Telestina Silanda (45) ameuawa kwa kuchinjwa na mwili kucharangwa na watu wasiojulikana akiwa amelala nyumbani kwake usiku wa kuamkia jana.
Ndugu wa marehemu, Charles Silanda alidai tukio hilo lilitokea saa mbili usiku ambapo watu wasiojulikana waliovalia “kininja” walipovamia nyumba yake na kumshambulia kwa panga na kumchinja.
Alisema kuwa mara baada ya kupata taarifa waliamua kukimbilia eneo la tukio ambapo walikuta shangazi yao ameuawa na waliofanya mauaji hayo wakiwa wametoweka.
Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Konrad Kauzeni alisema mwanamke huyo aliuawa kinyama, kwa kukatwa miguu yake yote miwili na kuitenganisha na mwili, kichwa na shingo.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kasha kuongeza kuwa ataenda kijiji hicho wananchi wapige kura za maoni ili kuwabaini wauaji hao.