Mwanamke amuua mumewe, amzika kimyakimya

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,446
Shimo-lenye-mtu.jpg

19 Jun 2018
MWANAMKE mmoja nchini Uganda, Dina Ainomugisha (45) amekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua mume wake, Gordon Ahimbisibwe na kumzika kwa siri huku akishirikiana na ndugu zake kwa kinachodaiwa ni ugomvi wa mali za familia.



Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Ibanda, Rogers Chebene amesema kuwa mmoja wa watuhumiwa ambaye alishiriki katika zoezi hilo aliamua kutoa taarifa kwenye uongozi wa Serikali ya Kijiji baada ya kukosa mgao wake wa fedha kama walivyokubaliana awali.



Baada ya kumuua, watuhumiwa wote wakishirikiana, walichimba shimo na kuuzika mwili wa marehemu usiku wa manane.



Watuhumiwa wengine walioshiriki katika tukio hilo wametajwa kuwa ni Keresensio Mwesigye ‘Kamwesi’, Experito Kacunguza, Stephen Mukama na Medrine Kabasiita ambao wote wameshakamatwa na jeshi la Polisi.



Taarifa zimeeleza kwamba, mwili wa Marehemu umechukuliwa na kupelekwa katika kituo cha Afya cha Ruhoko kwa uchunguzi zaidi.
 
Asili ya mwanamke,ni kuwa na roho ngumu

iwapo roho hiyo,itachanganyika na roho mbaya

Kinachofuata,ni unyama usiolezeka
 
Back
Top Bottom