Valentina asante, umefanikiwa kunitoa machimboni.
Hakuna suala la kuwezeshwa kwa mwanamke, mwanamke kama mwanamke anao utashi sawa na mwanaume kiasi kwamba anao uwezo wakusimamia mambo yake hata zaidi ya wanaume, suala la kusema hadi tuwezeshwe ndio tuna weza ni hoja dhaifu na haina mashiko katika katika dunia hii ya sasa kwasababu, wanawake tunauwezo na nguvu, maarifa nk. Angalia katika elimu je ni mabinti wangapi wanafanya vizuri je wameweze na nani ili hali masomo, walimu na mitihan vyote wanashiriki pamoja??
Pia hata maofisin kuna wanaume wangapi ni mizigo ili hali akina mama wanasimamia ofisi kwa ustadi mkubwa, je wamewezeshwa na nani???
Pia kuna wanawake wangapi wanaendesha maisha na kutafuta maisha na wameweza kuliko hata wanaume, je wamewezeshwa na nani???
ifahamike wazi dhana ya ufemisti ndio iliyomfungua mwanamke na kumfanya ajitambue kuwa anauwezo sawa sawa na binadamu mwingine. Na ni kweli mwanamke anaweza yeye kama yeye hakuna suala la kuwezeshwa, ikiwa mtu anasema lazima tuwezeshwe anapaswa kutoa ushahdi yeye amewazesha wangapi katika nyanja ipi.
Huwa naita inferiority complex, kuna wakati binadamu kaumbwa kuhamaki bila sababu hasa anapoona kazidiwa jambo fulan na mwanamke, hawezi kukubali matokeo atatafuta sababu ili tu kutaka kujaribu kumshusha katika level aliyokuwepo. wengi wao hudai mwanamke akifanikiwa anakuwa jeuri, hataki kushindwa nk, huwa najiuliza je hawa watu katika familia zao jinsi ya kike wote hawajafanikiwa au?? Maana wapo ambao wakiona mwanamke kafanikiwa hawaishi kusema, anajiuza, anategemea kuhongwa nk muulize ushawah kumuhonga? Au ashawah kukuuzia anabaki anajikanyaga.Wako wanaoamini kwamba mwanamke akifanikiwa kufika juu/kuweza/kuwezeshwa basi anaota mapembe kwakuonyesha dharau za wazi kwa wanaume. Hili unalionaje kwa upande wako?
Bila shaka mko vema na mwaendelea vema na majukumu yenu ya hapa na pale. Kwa wagonjwa ama mafadhaiko mbalimbali tunawaombea hali zirudi kua sawa....
Nisiandike mengi sana ya kuwachosha niende moja kwa moja kwenye swali langu ambalo leo nimekua interesting nalo japo hua nalisikia na limezungumzwa sana ila kwaleo nimependa kusikia kwa undani wake zaidi...
Kuna ule msemo kwamba "mwanamke akiwezeshwa anaweza"
Swali langu hapo ni kuwezeshwa kwa namna gani huko kunakozungumziwa? Ina maana pasipo kuwezeshwa ndio hatuwezi kabisa au mambo yataenda taratibu ama tutabweteka? Mimi sijui zaidi ila naomba mnifafanulie hapo.
Wanawake wenzangu hebu njooni tusemezane hili,ni kweli pasipo kuwezeshwa hatuwezi? Hatuwezi kusimama hata kidogo peke yetu bila upande wa pili kuwepo kutushika mkono?
Munkari, ICHANA, Apologise lady, Everline lank, Madame B, Blue G, sweet lady, Heaven Sent,na wengineo
Wanaume nanyi karibuni mtuambie nini mtazamo wenu katika hili?
walitaka kuwezeshwa wakawezeshwa wakawezesheka sasa viburi juuInawezekana unaingalia kauli hiyo kutoka angle ipi...Mwanzo wa kauli hiyo haikuwa na maana ya kuwadhalilisha kina mama ilikuwa ni kampeni dhidi ya wanawake....Kwa maana ya mwanamke akiwezeshwa anaweza hasa katika nyanja za kisiasa zamani kulikuwa hamna uwiano kati ya wanawake na wanaume katika nafasi mbalimbali na hao wachache waliojaribiwa kupewa nafasi hizo walifanya vizur ndo ukaja huo usemi wa mwanamke akiwezeshwa atawezana yakajitokeza mashirika kama women empowerment.....Ila nadhani mmewezeshwa hadi mnakaribia kutupita wanaume nadhani inahitajika jitihada za makusudi za kuwarudisha nyuma...Hakika.
Umenena vema kabisa bibie natamani wote wenye mawazo hasi wabadili fikra zao....Huwa naita inferiority complex, kuna wakati binadamu kaumbwa kuhamaki bila sababu hasa anapoona kazidiwa jambo fulan na mwanamke, hawezi kukubali matokeo atatafuta sababu ili tu kutaka kujaribu kumshusha katika level aliyokuwepo. wengi wao hudai mwanamke akifanikiwa anakuwa jeuri, hataki kushindwa nk, huwa najiuliza je hawa watu katika familia zao jinsi ya kike wote hawajafanikiwa au?? Maana wapo ambao wakiona mwanamke kafanikiwa hawaishi kusema, anajiuza, anategemea kuhongwa nk muulize ushawah kumuhonga? Au ashawah kukuuzia anabaki anajikanyaga.
Suala kubwa hapo ni inferiority complex na hakuna jambo lingine.
Lakin wapo wengine wanachukulia kawaida mafanikio ya mwanamke na wanasupport kubwa sana hasa ya mawazo ambazo huweza kumsaidia mwanamke kufikia malengo yao, "hao ni wanaume wa kweli"