Mwanamke adakwa na meno ya tembo

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
MENO%2BYA%2BTEMBO-1.jpg



POLISI Mkoani Morogoro inamshikilia mwanamke aliyatambuliwa kwa jina la Magreth Mosha (34) mkazi wa Kibaha, mkoani Pwani kwa tuhuma ya kukutwa na meno saba ya tembo katika nyumba ya kulala wageni iliyopo katika Manispaa ya Morogoro.

Meno hayo yalikutwa yameviringishwa kwenye mfuko wa salfeti na kufichwa mvunguni mwa kitanda katika chumba aliyofikia.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema hayo leo kuwa tukio hilo lilitokea Machi 28, Mwaka huu majira ya saa nane mchana eneo la mtaa wa Kingo, Manispaa ya Morogoro katika nyumba ya kulala wageni ya Miami Beach chuma namba 2 alichokuwa amepanga Magreth Mosha (34) mkazi wa Kibaha.

Kamanda Matei alisema askari Polisi kwa kushirikiana na wenzao wa TANAPA wakiwa doria walipata taarifa kutoka kwa watu wema na walipofika katika eneo la nyumba hiyo walimkamata mwanamke huyo na baada ya kufanya upekuzi katika chumba alichokodi ndipo walipomkamata na uthibitisho huo.


Magreth Mosha anashikiliwa na polisi kwa kukutwa na vipusa vya tembo
 
Kumbe neno kipusa utumika pia kwenye kumaanisha meno ya tembo. Nilidhani hutumika kumaanisha pembe ya faru tu. Ahsante mleta mada.
 
Alikua anapambana kuuaga umasikini.

ila atanyea debe si chini ya miaka mitatu hapo
Kuna jamaa alikutwa na kilo 21 za mirungi Moshi kala mvua sijui ya miaka 39 huyu sijui watamfanyaje ,ila sheria ni kitu cha ajabu anaweza akaachiwa huru tu
 
Sijawahi kusikia pembe ya faru ikiitwa kipusa. Nijuavyo ni ya ndovu tu.
Vizuri. Ila kama ndivyo hivyo basi kamusi ya TUKI nayo inatuchanganya kwani inaeleza kwamba kipusa ni pembe ndogo ya faru (rhino horn) na pia mwanamke mrembo/kidosho. Hivyo kwa kuwa specific kwamba ni pembe ya faru nikadhani za tembo hazihusiki.
 
Vizuri. Ila kama ndivyo hivyo basi kamusi ya TUKI nayo inatuchanganya kwani inaeleza kwamba kipusa ni pembe ndogo ya faru (rhino horn) na pia mwanamke mrembo/kidosho. Hivyo kwa kuwa specific kwamba ni pembe ya faru nikadhani za tembo hazihusiki.

Sijawahi isoma hiyo kamusi na kama nilivyoandika awali, ufahamu wangu kipusa ni pembe ya ndovu. Hii ya kuwa ya faru pia ni kipusa ndiyo nimejifunza kwenye huu uzi.

Hiyo maana nyingine nnaifahamu.
 
Uchunguzi ufanyike wa kutosha nina mashaka na namna mtuhumiwa alivyokamatwa, mzigo ulivyofichwa uvunguni na jinsi ulivyofungwa kwenye salfeti. Kuna dalili za kubambikiziwa zigo, umepanga gest jitu lina kuchomekea mzigo uvunguni ujui hili wala lile. Ningekuwa mm ningegoma gest si nyumba yangu, wakati naingia waliniona na na huo mzigo? So possible ni mwenye gest kautunza uvunguni maybe.
 
Sijawahi isoma hiyo kamusi na kama nilivyoandika awali, ufahamu wangu kipusa ni pembe ya ndovu. Hii ya kuwa ya faru pia ni kipusa ndiyo nimejifunza kwenye huu uzi.

Hiyo maana nyingine nnaifahamu.
Ahsante FaizaFoxy. Nahisi na wewe ni kipusa kwa hiyo maana nyingine. Aaah aah. Just kidding to brighten my day.
 
Back
Top Bottom