Mwanamichezo Amshambulia mama wa mtoto wake

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
13,096
22,621
Aliyekuwa mchezaji wa American football wa team ya New York Jets ,huko Marekani, kijana anayekwenda kwa jina la Zack stacy (umri wa miaka 30),amejikuta matatani baada ya aliyekuwa mpenzi wake, Kristin Evance (umri miaka 32),kupost mtandaoni video iliyorekodiwa na kamera za kiusalama ndani ya nyumba,ikimuonyesha katika tukio lisilo la kawaida na lisilokubalika la shambulio la mwili na domestic Violence.

Katika video ambayo aliipost Kristin mwenyewe katika mtandao maarufu wa tweeter inamuonyesha Stacy akimshambulia binti huyo mbele ya mtoto wao wa kiume (umri miezi 5) kwa kumpiga makofi na ngumi za kiume kisha kumnyanyua na kumtupa(Body slam) ukutani katika TV ambayo inavunjika na kumuangukia binti huyo ambaye alionekana wazi kukosa namna ya kujitetea na kuzidiwa nguvu, kisha kumnyanyua tena na kumtupa juu ya baby trainer na kumtupia kitu au vitu vinavyosadikika kuwa ni simu na vikolokolo kwa hasira mbele ya mtoto wake kichanga huku mtoto akilia kwa hofu kumuona baba yake akimshambulia mama yake na kuondoka kuelekea kusiko julikana hadi wakati video ikipostiwa na mama mtoto wake huyo.

Kristine amesema kwa sasa ameshatoa taarifa kwenye vyombo vya usalama na sheria na kupewa kinga ya kiusalama (restraining Order) dhidi ya mwanaume huyo na tayari vyombo vya usalama na wasamalia wema wapo katika harakati za kumsaka na kumtafuta maeneo mbali mbali ambapo anaweza kuwa ametokomea ili aweze kufikishwa katika vyombo vya sheria kujibu mashtaka hayo.

Alisema, “Amenipiga mara kadhaa kichwani, nilimsihi aache kwasababu mtoto alikuwa kwenye kochi futi chache kutoka alipokuwa akinipiga”alisema Kristin katika repoti aliyotoa polisi.
Baada ya shambulizi hilo Kristine alipata nafasi ya kuwapigia simu polisi na kuripoti kasha kuwasiliana na hospitali kwaajiri ya msaada wa kimatibabu.

Pia Kristin aliweka wazi kuwa hii si mara ya kwanza kwa Zack kumshambulia na kusema alishawahi kumshambulia kipindi akiwa na ujauzito wa mtoto wao huyo kwa kumshambulia mfululizo bila dalili ya kuacha.

Pia Kristine alisema kuwa Zack,kwa hiyari yake alishawahi kufika hospitali kwaajiri ya matibabu maalumu ya akili kipindi cha mwezi March 2021 na alikuwa akitumia dawa za kutibu hali yake.

Akizungumza na daily mail.com,Jumatano hii,Kristin alibainisha kuwa hadhani kuwa Zack anapitia hali aliyo nayo kama matokeo ya shughuli zake za kimichezo ila pengine zimechangia yeye kuwa na hali ya jazba na hasira.

Ripoti kutoka kwa wasimamizi wa hospitali wanasema baada ya shambulizi hilo Kristin alipata uvimbe wa nje sehemu zilizopata majeraha, mikwaruzo na michubuko pamoja na majeraha madogo maeneo ya kichwani.

Couple hii ilikutana January 2019 wakati wakifanya kazi kitongoji kimoja cha Memphis, na hawakuwa kimahusiano ya mapenzi hapo awali hadi miezi kadhaa baadae mwaka huo huo.
Kristin amemuelezea Zack kuwa alikuwa ni mwanaume mcheshi,mtulivu na walikuwa na vingi vya ufanano na mambo yalianza kwenda kombo walipoanza kutofautiana mwezi December 2019 ujauzito wa Kristin ulipotoka. “tuliamua kutengana sababu ya tofauti zetu ndogo ila baadae tukarudiana.
Kristine alipata tena ujauzito mwaka huu 2021 na wakati huo huo Zack alikwenda Florida mwezi April kwa shughuli zake na mambo yakawa si sawa tokea wakati huo. Shida ilianza zack alipokuja mtembelea yeye na mtoto majira ya saa nane za mchana siku ya jumamosi.

Wawili hawa wamekuwa wakiishi mbali tokea mwezi August mwaka huu. Alipofika alianzisha mazungumzo kuhusu tukio lililotokea mwezi September 2020 ambalo lilihusu Kristin kukutana na Mshauri wa maswala ya kifedha wa Zack wakizungumzia juu ya mashaka ya afya ya akili ya zack na ndipo ghafla akafyatuka na kuanza kumshambulia Kristine kwa kipigo kizito.


Chanzo cha habari :

 
Zack Stacy
Screenshot_20211119_005518.jpg
 
Naona Joyce Kiria unapost harakati zako za kutetea haki za wanawake.Hongera
Hiyo haina uhusiano na haki za mwanamke moja kwa moja.

Inauhusiana na kukemea ukatili dhidi ya wengine (Bullying). Anaweza kuwa anaefanyiwa ni mtoto, mwanaume, mwanamke, mzee au mgonjwa.

Yaani kwa kifupi jamaa hapo hakutakiwa kutumia nguvu zote hizo kwa huyo mkewe maana kwanza anaonekana ni mpole, na ana staha huoni akimuwashia moto au kumpandishia sauti zaidi ya kumsihi aache kumshambulia.

Sasa ndugu yangu wewe unaona ni swala la kijinsia tu kabla ya jinsia kwanza kuna ubinadamu me natazama kwanza ubinadamu ndo maana hata akifanyiwa ukatili yoyote yule nitakemea.

Uonevu sio swala la kijinsia ni la kitabia. Jamaa amemuoenea huyo mwanamke na amemkosea heshima mtoto wake.

Anastahili adhabu kali sana.
 
Back
Top Bottom