Mwanajeshi wa Urusi awapiga wenzake wanane risasi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
MWANAJESHI mmoja wa Urusi amewapiga risasi wanajeshi wenzake wanane na kuwajeruhi vibaya wengine wawili katika kambi ya kijeshi iliopo mashariki kulingana na maofisa.

Askari huyo, Ramil Shamsutdinov ambaye alikamatwa huenda alikuwa akiugua tatizo la kiakili.

Tukio hilo lilifanyika katika kitengo cha kijeshi nambari 54160 katika kijiji cha Gorny sio mbali na mji wa Chita Ijumaa jioni.

Kisa hicho kilitokea mwendo wa saa 12:15 kulingana na kamati ya uchunguzi ya Urusi.

Wizara ya Ulinzi ilisema risasi zilifyatuliwa wakati wa kubadilishana zamu katika eneo la Transbaikal. Shamsutdinov kuruta aliwaua maafisa wawili na wanajeshi wenzake sita.

Vyombo vya habari nchini Urusi vimeripoti kuwa mshukiwa huyo aliwalenga waathiriwa katika vichwa.

Tume maalumu inayoongozwa na Naibu Waziri wa Ulinzi, Andrey Kartapolov inaelekea eneo hilo ili kuchunguza mauaji hayo.

Kitengo hicho cha jeshi nambari 54160 kinahifadhi makombora. Kina makombora ya Iskander ambayo yana uwezo wa kubeba vichwa vya kinyuklia.

Huduma za jeshi ni lazima nchini Urusi kwa wanaume wote walio kati ya umri wa miaka 18-27.

Wao huhudumu kwa miezi 12 na baadaye wanaweza kusaini kandarasi za kitaalam ili kuendelea kuhudumu katika jeshi.

Miaka ya 2000, makundi ya haki za kibinadamu yaliripoti ghasia na unyanyasaji kwa jina ”dedovshchina” dhidi ya makurutu wapya katika jeshi la Urusi.

Lakini katika miaka ya hivi karibuni, Urusi inajivunia kuliimarisha jeshi lake na kuondoa unyanyasaji.


Chanzo: Mtanzania
 
... kichaa kinagundulika baada ya kuuwa wenzake 8! Hatari sana.
 
Kawaida tu hiyo jeshini,hasa hutokea wamajeshi kukaa deployment muda mrefu bila mapumziko ya kutosha...
 
Back
Top Bottom