GE2025 Mwanaisha Mndeme ahidi Mikopo ya 10% na Elimu ya Ujasiriamali kwa Wajasiriamali Wadogo Jimbo la Kigamboni

GE2025 Mwanaisha Mndeme ahidi Mikopo ya 10% na Elimu ya Ujasiriamali kwa Wajasiriamali Wadogo Jimbo la Kigamboni

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
505
Reaction score
887
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigamboni kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Wakili Mwanaisha Mndeme, amefanya kikao cha ndani na wakazi wa Mjimwema ikiwa ni sehemu ya kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba 2025.

Katika kikao hicho, Mndeme alikutana na makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo mama lishe, wajasiriamali, waendesha bodaboda pamoja na wabangua mawe, ambapo aliwasilisha vipaumbele vyake vya maendeleo ambavyo analenga kuvitimiza endapo atachaguliwa kuwa Mbunge wa Kigamboni.

Mgombea huyo alieleza kuwa iwapo atapata ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo hilo atahakikisha utolewaji wa mikopo ya asilimia 10% kutoka Halmashauri inawafikia walengwa bila ubaguzi, elimu ya ujasiriamali na elimu ya sheria kwa wajasiriamali wadogo ili kuwasaidia kufanikisha shughuli zao kwa ufanisi zaidi.

Wakazi wa Mjimwema waliipokea kwa matumaini mikakati ya Mndeme, huku wengi wakionesha kutaka mabadiliko ya kiuongozi yatakayoleta maendeleo ya kweli katika jamii yao

Screenshot 2025-10-16 172934.png
Screenshot 2025-10-16 172943.png
 
Back
Top Bottom