Mwanahalisi: Maige anatafuta nini Barrick?

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Maige anatafuta nini Barrick?

Na Mwandishi Maalum

EZEKIEL Maige aweza kuwa mwigizaji au mtendaji wa dhati. Bali kwa sasa hakuna awezaye kujua nia, shabaha na uwezo wake.

Waziri huyu wa maliasili na utalii anasema ameamua kupambana na kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya African Barrick Gold (ABG).

Hii ni kampuni ambayo serikali ya Chama Cha Mapinduzi imeipa migodi mikubwa nchini na haikohoi kuhusu nyendo zake.

Lakini Maige anasema anafanya kampeni ili kampuni hiyo inayomiliki migodi minne mikubwa nchini, isiendelee kupewa leseni za uchimbaji madini, hasa katika maeneo ya wachimbaji wadogo.

Ameuambia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kakola, kata ya Bulyanhulu, wilaya ya Kahama, Shinyanga kwamba anasikitika hawakumshirikisha katika hatua za mwanzo za kupambana na Barrick, lakini anasema “sasa ninajua cha kufanya.”

Anasema atapinga uamuzi wa serikali yake kutoa leseni inayopora haki za wapigakura wake.

Maige anajua nguvu ya Bulyanhulu. Wakazi wengi wa kata ya Bulyanhulu walimnyima kura katika uchaguzi mkuu uliopita. Wachunguzi wa mambo wanasema anatafuta “mahali pa kuingilia” kujenga mahusiano mapya.

“Kuna mwakilishi yeyote wa Barrick katika mkutano huu?” aliuliza waziri Maige katika mkutano wa hadhara.

“Maana nataka ujumbe huu uwafikie. Kampuni hii (Barrick) sasa inataka kutuchonganisha kwa wananchi ili waichukie serikali yao. Kila mahali wanataka wachukue wao. Ukienda Mwazimba ni wao, Sekenke ni wao, sijui wapi ni wao,” alilalamika.

“Pale Mwazimba kuna mgogoro; tayari wamepata leseni wanataka kuhamisha vijana wanaochimba. Niliwaambia mbona ninyi mna maeneo makubwa tu,” alisema.

Hapa ndipo kuna shaka na hata utata. Maige ana ubavu wa kuamrisha serikali yake?

Kampuni ya Barrick Gold Corporation ya Canada ambayo kupitia kampuni yake tanzu ya ABG inamiliki migodi minne, imerithi mali na matatizo ya makampuni yaliyoanza kuchimba dhahabu nchini.

Barrick inamiliki mgodi wa Bulyanhulu baada ya mwaka 1999 kununua hisa zote za Sutton Resources ya Canada ambayo kupitia kampuni tanzu ya Kahama Mining (KMCL), ilianza kuchimba madini mwaka 1996. Mgodi huo ulianza uzalishaji mwaka 2001.

Barrick pia ilinunua hisa zote za mgodi wa North Mara kutoka Placer Dome mwaka 2006 ulioanza uzalishaji mwaka 2002. Awali mgodi huo ulikuwa unamilikiwa na Afrika Mashariki Gold Mine (AMGM) ya Australia.

Vilevile Barrick ilitwaa mgodi wa Tulawaka ulioanza uzalishaji mwaka 2005 na Buzwagi mwaka 2009.

Pamoja na Barrick kumiliki maeneo hayo yanayozalisha mamilioni ya aunzi za dhahabu kwa mwaka, bado inakodolea macho maeneo ya wachimbaji wadogo kama Mwazimba, Nyangalata, Nyamalata na Nyakagwe (Geita).

Maige anasema hakubaliani na hatua ya wizara ya nishati na madini kuipa leseni ya utafiti wa madini, kampuni ya Mikumi Exploration iliyosaini mkataba na Barrick, mmiliki halali wa leseni ya kutafuta madini kwenye eneo la Jomu na Mwazimba, wilayani Kahama.

ABG inalalamika kwamba eneo lake limevamiwa na kikundi cha Kasi Mpya Gold Mining Corporative Society (KAGAMICO). Lakini akiwa Mwazimba, kata ya Bugarama, Maige alipinga kuondolewa kwa kikundi hicho.

“Mimi nitafanya kazi ya kuwatetea. Niko tayari kulipa gharama yoyote itakayoendana na kusema ukweli katika jambo hili,” alisema Maige huku akishangiliwa kwa nguvu na wachimbaji wadogo.

Tayari Maige ameandika barua kwa waziri wa nishati na madini, William Ngeleja kumwomba asitishe mpango wa kuhamisha wachimbaji wadogo kutoka Mwazimba.

Maige anacheza siasa?

Chanzo: MwanaHalisi Gazeti toleo na. 235
 
viva maige, go please go kutetea maslahi ya waliokuajiri kuwa mbuge. hope tu see changes very soon.
 
viva maige, go please go kutetea maslahi ya waliokuajiri kuwa mbuge. hope tu see changes very soon.

Ndugu yangu unahadaika kirahisi hivi? utajuaje kama ni mchezo wa kuigiza? ukishangaa ya Maige utaona ya Magufuli. Endelea kutazama hiyo movie.
 
Maige hana lolote, alitaka kuiba eneo la barrick ambalo wametumia Bil2 kufanya utafiti kwa kigezo cha yeye kuwa waziri akashindwa. Baada ya kushindwa akaamua kupambana na Barrick kwa kutumia political influence yake hadi wapokonye, na kampuni liyokuwa inataka hilo eneo inaitwa Kasi Mpya na yy ni mmoja wa wamiliki. Kwa habari zaidi Ofisi ya Madini Kama na Wizara ya Nishati na Madini Dar.
Afu ofisa aliyeambiwa kuliiba hilo eneo ni wa Kahama, sijui kama atakuwepo kazini maana baada ya kushindwa wakambabikia kapewa rushwa na Barrick.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom