Dark Angel
JF-Expert Member
- Sep 12, 2013
- 212
- 220
Mwanahabari aliyesaidia kundi la al-Shabaab kuua wanahabari wenzake nchini Somalia ameuawa.
Hassan Hanafi ameuawa kwa kupigwa risasi mapema asubuhi baada ya kuhukumiwa kifo na mahakama ya kijeshi nchini humo.
Hassan Hanafi, alipatikana na hatia ya kuwaua Sheikh Noor Mohamed Abkey (mhariri wa shirika la habari la SONNA),
Sa'id Tahlil Warsame (mkurugenzi wa HornAfrik), na MukhtarMohamed Hirabe (mkurugenzi wa Radio Shabelle), na wanahabari wengine kadha.
Alikamatwa nchini Kenya Agosti mwaka 2014 na kupelekwa Somalia mwishoni mwa mwaka jana.
Alihukumiwa kifo na mahakama ya kijeshi ya ngazi ya chini nchini Somalia tarehe 3 Machi.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, maafisa wa jeshi wamesema mwanahabari huyo alikiri mauaji ya wanahabari watano.
Chanzo: BBC