informer 06
Senior Member
- May 11, 2024
- 122
- 111
Mwanafunzi wa sheria, Onesmo Mathew, amezindua kitabu chake kipya kiitwacho Watanzania na Sheria, ambacho kinalenga kuwasaidia wananchi wanapokumbana na changamoto za kisheria.
“Kitabu hiki kitaleta mwongozo kwa wananchi ili wajue sehemu ya kuanzia, hususan katika masuala ya madai na jinai,” alisema Onesmo wakati wa uzinduzi uliofanyika tarehe 22 Agosti 2025.
Akizungumza katika hafla hiyo, Onesmo ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Sheria ya Dar es Salaam, alisema kuwa changamoto nyingi za kisheria zimekuwa zikiikumba jamii, lakini wananchi wengi hawajui hatua za kuchukua, hasa wanapotaka kufungua mashauri mahakamani.
View: https://youtu.be/ZLcUkxJ2MdI?si=PxmQt6bnkFHpzkPD
Aidha, alieleza kuwa kitabu hicho kinatoa mwanga kwa wananchi kuelewa haki zao wanapokamatwa. Alibainisha kuwa kuna haki muhimu zinazopaswa kuzingatiwa wakati wa ukamataji, na kupitia kitabu hicho wananchi watapata uelewa mpana zaidi kuhusu suala hilo.
Kwa upande wake, Mratibu wa THRDC, Wakili Onesmo Olengurumwa, alisema kuwa kwa sasa kumekuwepo na changamoto ya wananchi wengi kutojenga tabia ya kusoma na kuandika. Alisisitiza kuwa ni muhimu kwa jamii kukuza utamaduni wa kusoma ili kupata maarifa zaidi, kwani maandiko bora hujengwa juu ya tafiti na mawazo yenye mashiko.
Imeelezwa pia kuwa kitabu hicho kimegusia masuala mbalimbali ikiwemo ndoa, ardhi, ukamataji na mambo mengine kadhaa yanayojitokeza mara kwa mara katika jamii.