Mwanafunzi wa Kidato cha tatu ajinyonga

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,641
22,017
Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu katika Shule ya Sekondari Nyanungu Tarafa ya Ingwe wilayani Tarime mkoani Mara, Charles Chacha (19), amekutwa amejinyonga chumbani kwake kwa kutumia kamba ya katani.

Diwani wa kata hiyo ya Nyanungu, Mang’enyi Ryoba amesema Chacha alijinyonga Februari 23, mwaka huu usiku, baada ya yeye na wenzake wawili wa kike kupewa barua shuleni siku hiyo ya adhabu ya kutodhudhuria shuleni kwa siku 14.

"Sababu ya kupewa barua hiyo ya adhabu haijafahamika. Tunafutilia kujua tatizo la wanafunzi hao lilikuwa ni nini.Tulitoa taarifa kituo cha Polisi Kegonga na Nyamwaga ambao walifika na kuuchukua mwili wa marehemu huyo,” alisema Diwani Mang’enyi.

Kamanda wa Polisi Tarime/ Rorya, Gemini Mushi alithibitisha kutokea kwa kifo hicho na kueleza kuwa chanzo kinachunguzwa.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Wilaya.
 
Kwa miaka 19 alipaswa kuwa f6. Adhabu tu imfanye ajinyonge? Kwani walisimamishwa kwa wiki 2 pasipo wazazi kujua? Jamani, watoto wafundishwe na wazazi kumwogopa Mungu. Wanadhani kujiua ni kupumzika kumbe ndipo kulia na kusaga meno kunaanza.
 
Kula la hero huko aliko, uwiiiii uwiiii
 
Walimu wawe wanatoa ushauri nasaha baada ya kutoa adhabu

Walimu wengi siku hizi wamepinda, wamechoka wanaona njia rahisi ya kuondokana na usumbufu ni kumsimamisha mwanafunzi masomo au kufukuza, swala la unasihi kwao ni mzigo
 
Kwa miaka 19 alipaswa kuwa f6. Adhabu tu imfanye ajinyonge? Kwani walisimamishwa kwa wiki 2 pasipo wazazi kujua? Jamani, watoto wafundishwe na wazazi kumwogopa Mungu. Wanadhani kujiua ni kupumzika kumbe ndipo kulia na kusaga meno kunaanza.
Nahisi hata balehe inachangia kuingia Katika matatizo Kama hayo
 
Kwa miaka 19 alipaswa kuwa f6. Adhabu tu imfanye ajinyonge? Kwani walisimamishwa kwa wiki 2 pasipo wazazi kujua? Jamani, watoto wafundishwe na wazazi kumwogopa Mungu. Wanadhani kujiua ni kupumzika kumbe ndipo kulia na kusaga meno kunaanza.
amekwenda kujipeleka mwenyewe kwenye kulia na kusaga meno mwache ameamua kujiwahisha kuzimu
 
Inasemekana hiyo kamba aliyojinyongea inahitajika sana kwenye masuala ya Sayansi ya Kiafrika
halafu hiyo kamba tena imemkwida mwingine wa harare ruvuma naye ni mtumzima kajonyongea nayo kisa amechoka kudai hela zake kwa watu wasiotaka kumlipa yaani binadamu wanashangaza sana kweli mtu unaamua kujimaliza kwa vitu ambavyo havina thamani ya uhai wako aisee
 
Back
Top Bottom