Mwanafunzi wa DRC auawa India

Babu wa Kambo

JF-Expert Member
May 2, 2016
559
808
160525120633_drc_student_kiliing_512x288_bbc_nocredit.jpg

Kundi moja la Balozi za Bara Afrika mjini Delhi limeitaka India kuahirisha sherehe moja ya kitamaduni kufuatia kuuawa kwa mwanafunzi mmoja kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wiki iliopita.

Masunda Kitada Oliver alipigwa hadi kufariki na kundi moja la wanaume wa Kihindi Ijumaa iliopita baada ya majibizano mjini Delhi.

Watu wawili wamekamatwa kufuatia kisa hicho.

Balozi hizo zimesema kuwa hazitaki kushiriki katika kuadhimisha siku ya Afrika siku ya Alhamisi kufuatia misururu ya mashambulizi dhidi ya wanafunzi kutoka Afrika.

''Hii ni kwa sababu jamii ya Kiafrika nchini India ,wakiwemo wanafunzi wanaendelea kuomboleza kuwaenzi wanafunzi wa Afrika waliouawa akiwemo bwana Oliver", alisema Alem Tsehage Woldremariam, kiongozi wa mabalozi wa Afrika nchini India.

Mnamo mwezi Februari, mwanafunzi mmoja wa Tanzania alipigwa na kuvuliwa nguo na kundi moja katika mji wa Kusini wa Bangalore.

CHANZO: BBC Swahili
 
Hiyo ndio india bwana ukileta jeuri wanakuvua mpaka CHUPI, na huwenda wakakunanihiii kule nyuma.....
 
HHHHHHHHHao mabalozi wa afrika si wangetangaza tuu mgogoro wa kidiplomasia na INDIA, na kuzuia wanafunzi wa kiafrika wasiende kusoma India kwani ni lazima!? maana wahindi wamezidi!
 
Mimi na wahindi sitakagi kabisa mazoea nao,muhindi kama walivyo wao simfagilii hadi nimeona nina maslahi nae vinginevyo namwona pumba tu,believe me..ukimuona muhindi anajinyenyekeza kwako jua una maslahi kwake,hasa kwenye biashara akija kwa dharau kwangu atazipata akija kistaarabu tunaenda sawa wana ubaguzi sana hawa ponjoro.
 
Back
Top Bottom