kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,083
ZIMEBAKI siku chache kwisha kwa muda wa utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli kuhusu madawati katika shule za msingi na sekondari. Rais Magufuli ameagiza shule zote za msingi na sekondari ziwe na madawati na ifikapo Juni 30 kusiwe na mwanafunzi atakayekaa chini darasani.
Wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa halmashauri wamepewa jukumu la kuhakikisha kuwa agizo hilo linatekelezwa na yeyote atakayeshindwa yupo hatarini ‘kutumbuliwa’. Wananchi wanaunga mkono juhudi za serikali kuhakikisha wanafunzi wanakaa kwenye madawati darasani. Shule kadhaa zimepata msaada wa madawati. Licha ya changamoto katika utekelezaji wa agizo la JPM, limesaidia wananchi wengi waliokuwa mitaani kupata ajira za muda zikiwemo za kukata vyuma na kuranda mbao.
Katika mkoa wa Dodoma kuna juhudi zinaendelea katika halmashauri saba za wilaya hizo kuhakikisha agizo hilo la Rais linatekelezeka. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) George Simbachawene anasema wakuu wa Mikoa na wilaya ambao watashindwa kukamilisha agizo la kila shule kuwa na madawati ifikapo Juni 30, mwaka huu hali zao zitakuwa mbaya.
“Kuanzia Juni 30, mwaka huu hatutaki kuona mtoto akiwa amekaa chini. Kila mtendaji anatakiwa asimamie jambo hilo kwa nguvu zote, ikiwa hata kwa kutumia rasilimali kwa ajili ya kumaliza changamoto hizo.Kopeni hata za kununua madawati ili watoto wetu wasikae chini. Wakuu wa mikoa na wilaya watakaoshindwa kutimiza hilo hali zao zitakuwa ni mbaya. Kama umeshindwa kuwa na madawati, mkuu wa mkoa, wilaya, mkurugenzi na ofisa elimu wote hamtoshi,” anasema Simbachawene.
“Haiingii akilini mtoto kukaa chini katika karne hii, hatutunzi viti, madawati hayakarabatiwi. Dawati linakaa chumba cha vumbi lazima litavunjika tu. Kila halmashauri ihakikishe inakuwa na madawati ya kutosha kwa shule zote,” anasema. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana ametoa agizo kwamba, madawati ambayo yapo tayari yapelekwe shuleni ili wanafunzi waanze kuyatumia.
Rugimbana anayasema hayo wakati anatembelea karakana za kutengeneza madawati katika wilaya za Chemba na Kondoa. Kwa mujibu wa kiongozi huyo, kuna matumaini mkoa wa Dodoma utatimiza agizo la Rais Magufuli ifikapo Juni 30. “Vizuri kama madawati ambayo yapo tayari yapelekwe shuleni kwa ajili ya wanafunzi kukalia. Shule ya kwanza ambayo mtapeleka madawati niiteni ili nije nione agizo la Rais linavyotekelezwa,” anasema Rugimbana.
Anasema wilaya ya Chemba inaonekana kufanya vizuri katika utekelezaji wa agizo la Rais kwa kuwa vifaa vipo na mafundi wapo kazini hivyo kudhihirisha kuwa kazi hiyo itakamilika mapema. Wilaya ya Chemba Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Ramadhani Maneno anasema kuna karakana sita zinazotumika kutengeneza madawati na wanaamini kazi hiyo itafanikiwa kwa asilimia 100. Anasema Chemba ina upungufu wa madawati 9,400.
Kwa mujibu wa Maneno vifaa vyote kwa ajili ya kutengenezea madawati zikiwemo mbao vipo. Anasema changamoto kubwa ni kukatika katika kwa umeme hali hivyo kusababisha kazi hiyo kukwama mara kadhaa. Maneno anasema Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia ametoa Sh milioni 20 kutoka Mfuko wa Jimbo kwa ajili ya madawati. Rugimbana ameagiza juhudi ziongezwe katika utengenezaji madawati wilayani Kondoa.
“Nilichokiona Kondoa hamjakusanya mbao zote kwa ajili ya utengenezaji madawati. Mkiendelea kidogo kidogo hivyo hamtafika. Ongezeni mafundi zaidi ili muweze kufikia lengo hilo,” anasema. Rigimbana anataka Kondoa wahakikishe madawati yaliyo tayari yanapelekwa shuleni wanafunzi wayatumie. “Huku tunatengeneza, huku tunagawa, tutafika tu,” anasema.
Wilaya ya Kondoa Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Shaban Kisu anasema kazi hiyo inaendelea vizuri na kwamba, wilaya ya Chemba wamewauzia mbao kwa bei nafuu. Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa wilaya, wana matumaini kwamba watakamilisha utengenezaji wa madawati kama ilivyopangwa. Mkurugenzi Kondoa Vijijini, Hussein Ngaga anasema, wilaya hiyo ina upungufu wa madawati 11,817 na wana matumaini makubwa kuwa agizo la Rais Magufuli litatekelezeka.
Wilaya ya Kongwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Bituni Msangi anawataka wananchi wa wilaya hiyo kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ikiwa na pamoja kutumia nguvu zao zitakazowezesha upatikanaji wa madawati badala suala hilo kuachiwa serikali peke yake. Msangi anasema anatoa mwito kwa wananchi kusaidia uvunaji wa miti inayotengenezwa madawati na pia washiriki kikamilifu kuchangia nguvu zao au kutoa fedha ili kazi ikamilike katika muda uliopangwa na Rais Magufuli.
Anasema ili kuhakikisha azma hiyo inatekelezeka ni muhimu wananchi wa wilaya hiyo wakiwemo na wadau wa elimu washirikiane na serikali ili kuwaondolea wanafunzi kero hiyo ya kukaa chini inayowasababishia watoto wengi kufanya vibaya katika masomo au kuathirika kiafya. Msangi anasema, ameguswa na mchango wa mkazi wilayani humo Saimon Binde aliyetoa madawati 63 kusaidia kukabili upungufu uliopo.
Binde anasema kwa kuwa yeye ni mdau wa elimu na mkazi wa kijiji cha Tubugwe, ameguswa na kuamua kutengeneza madawati 63 na amemkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kongwa. Binde anasema kutokana na adha wanayoipata wanafunzi shuleni ya kukaa chini kwa sababu ya ukosefu wa madawati Watanzania na wadau wa elimu wanapaswa kuelekeza nguvu zao kuchangia kwa hali na mali kumaliza kero hiyo.
Anasema amejitolea madawati ili wanafunzi katika shule ya msingi Tubugwe Kibaoni wafanye vizuri katika taaluma. “Mimi kama mzazi nimeona nisaidiane na serikali ya awamu hii ya tano ambayo imesema inataka kuhakikisha watoto wote kwenye shule zetu hakuna mtoto ambaye atakayekaa chini kwa ajili ya kukosa madawati ndiyo maana na mimi nimeamua kuunga mkono jitihada hizo kuondoa kero hiyo ya ukosefu wa madawati mashuleni na watoto wetu waweze kufanya vizuri kimasomo,” anasema Binde.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Tubugwe Kibaoni, Hadija Mohamed anasema shule hiyo ina wanafunzi 584 wa darasa la kwanza hadi la saba na 128 wa shule ya awali hivyo jumla kuna watoto 712. Mwalimu Mohamend anasema, wanafunzi wote wa shule ya awali wanakaa chini darasani. Anasema, shule hiyo inahitaji jumla ya madawati zaidi ya 366 ili kuondoa kero ya ukosefu wa madawati. Wilaya ya Mpwapwa Katika wilaya ya Mpwapwa kuna upungufu wa madawati 6,586 kwa shule za msingi na sekondari.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Mohamed Maje anasema katika harakati za kumaliza changamoto ya madawati hadi Mei 30 mwaka huu halmashauri hiyo ilikuwa imetengeneza madawati 9,500. Hadi wakati Rais Magufuli anatoa agizo, halmashauri hiyo ilikuwa na upungufu wa madawati 16,086 katika shule za msingi na sekondari. Maje anasema watahakikisha agizo hilo linatekelezwa katika muda uliopangwa kwa kushirikisha jamii, wadau wa maendeleo na serikali.
Anasema mikakati iliyowekwa na halmashauri ni kuvuna baadhi ya miti , kuchana mbao kwa kuwatumia wafungwa wa Gereza la Ilolo, kutengeneza madawati na kuyagawa katika shule zenye upungufu mkubwa wa madawati. Wilaya ya Bahi Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Francis Mwonga amewataka watendaji wa wilaya hiyo kuendelea kushirikiana na ili kumaliza tatizo la upungufu wa madawati ifikapo Juni 30 mwaka huu.
Anasema wilaya hiyo ina upungufu wa madawati 5,600 na tayari mikakati imewekwa ili kufikia Juni 30 kila mwanafunzi awe anakaa kwenye dawati kama ilivyoagizwa na Serikali. “Tunataka agizo la serikali litekelezwe katika wilaya yetu kila kiongozi awe Diwani, Ofisa Tarafa, Mtendaji wa Kata na hata wananchi katika maeneo yenu angalieni upungufu uliopo wa madawati na juhudi za kumaliza upungufu huo,” anasema Mwonga.
Wilaya ya Chamwino Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Farida Mgomi anasema juhudi za kukamilisha kazi hiyo zinaendelea na kwamba, wanaamini agizo hilo watalitekeleza katika muda uliopangwa. Mgomi anasema kazi hiyo ilianza kwa kutumia vijiji vilivyokusanya mapato kwa wingi ikiwemo misaada kutoka kwa wabunge , asasi zisizo za kiserikali, wadau wa elimu na wananchi.
Anasema wametenga vituo viwili vya utengenezaji wa madawati, Chamwino na Mvumi Misheni na kwamba, vyote vinategemea uvunaji wa mbao kutoka msitu wa Chamwino. “Shule zetu zote zilizopo kwenye wilaya ya Chamwino kwa ujumla zina upungufu wa madawati 10,518 na kwa jitihada zetu tutakamilisha hili “anasema Mgomi. Anasema miongoni mwa miti wanayoivuna katika msitu wa Chamwino imeanguka yenyewe kutokana na mvua na upepo.
Mgomi anasema, wakati kazi hiyo inaendelea wamekamata mbao 200 zilizovunwa kinyume na sheria na zote wamepeleka zitumike kutengeneza madawati. Ofisa Misitu wa Wilaya hiyo Saidi Msemu anasema Kamati ya Halmashauri imejizatiti kukabiliana na changamoto ya madawati kwa kukata mti na kupanda miti. “Tunaendelea kuhamasisha upandaji miti na mpaka sasa tumefanikiwa kupanda miche 4,246 na tumeisambaza kwenye shule za msingi zilizopo kwenye Wilaya yetu,” anasema Msemu.
Halmashauri ya Manispaa Dodoma Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma imepanga kutengeneza madawati 10,000. Katika halmashauri hiyo kuna upungufu wa madawati 11,000. Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Azimina Mbilinyi anasema wamejipanga kufanikisha lengo hilo kwa kushirikiana na wadau. Zaidi ya vijana 200 mafundi seremala kutoka maeneo ya Jimbo la Dodoma Mjini wamepata ajira kupitia kazi hiyo.