MAKOLE
JF-Expert Member
- Feb 5, 2012
- 618
- 280
Habari kutoka Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro zinasema kwamba Mwanafunzi MWAJUMA A. VUZO wa kidato cha Tatu katika shule ya sekondari Makanya amepigwa na baba yake mzazi hadi kusababishiwa maumivu makali na hatimaye Jumamosi ya tarehe 14/2/2015 alifariki dunia na kuzikwa leo 16/02/2015.
Habari zinasema kwamba Baba Mzazi wa mtoto huyo aliamua kumpiga binti yake kwa sababu ya kukaidi amri ya mzazi huyo ya kumtaka aolewe, jambo ambalo marehemu alilipinga kwa kuwa alipenda kuendelea na masomo.
Aidha, kabla ya kifo chake, marehemu aliwahi kwenda shuleni baada ya kipigo ambapo alianguka ghafla na akapelekwa Hospitali ya wilaya ya Same ambapo alipatiwa Rufaa kwenda KCMC na kugundulika kuwa maini na vitu vingine vya ndani viliharibiwa vibaya hali ambayo ilisababisha atapike mapande ya damu.
Baba wa marehemu ametoroka na hadi sasa hajapatikana na msako mkali unaendelea. Tunamuomba Mungu ailaze roho isiyo na hatia ya mwanafunzi Mwajuma