tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Ahmed Makarani amethibitisha tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Qash iliyopo wilayani Babati, mkoani Manyara, Yohana Konki (17) kwa madai ya wizi wa kishkwambi.
Soma pia: Wizi Shule ya sekondari Kwa Shungu Ifakara
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo leo Agosti 17, 2025, Kamanda Makarani amesema tukio hilo limetokea saa 10 alfajiri ya Agosti 16 shuleni hapo ambapo wanafunzi 11, msimamizi na mlinzi wa shule hiyo wanashikiliwa kwa uchunguzi kufuatia kifo cha mwanafunzi huyo.
Kamanda Makarani amesema kuwa chanzo cha kifo cha mwanafunzi huyo ni baadhi ya wenzake kumpiga kwa kumtuhumu ameiba simu aina ya tablet baada ya majibu aliyoyapata mwanafunzi mmiliki wa simu hiyo baada ya kwenda na wenzake kwa mganga wa kienyeji na kupiga ramli chonganishi ili kumbaini mwizi.
Source: EastAfricatv