Kuna taarifa kutoka chanzo kwa mtu wangu wa karibu aliyepo chuoni hapo kwamba mwanafunzi wa kike amefariki jana baada ya kukanyagwa na wenzie kwa kile kilichoelezwa ni kukimbilia kuwahi seat wakati wa kufanya mitihani.
Kinachonisikitisha ni kwamba, hawa ni wanafunzi watu wazima na wengine wana waume/wake na watoto lakini hawajastaarabika hadi kufikia kumuua mwenzao katika purukushani za kuwahi viti. Tena ni wanafunzi wanaotarajia kumwaliza chuo mwaka huu sio hata first year kwamba utasema bado wanao usekondari ndani yao, na inasemekana ni wanaosomea ualimu..what a shame.
Na pia nashangaa sana kwamba hata ST Augustino wana matatizo ya kutokuwa na seat za kutosha kwa ajili ya wanafunzi wao? is it fair?, mbona ada inalipwa kubwa na chuo kina wafadhili? mi nilidhani haya mambo ya kusoma mmesimama au nje ya madirisha yao tu udsm. Mbona hatuna ustaarabu kwenye elimu jamani.
Mwisho natoa pole kwa familia ya huyo marehemu na Mungu aiweke pema roho yake. Amen.
Jamani fedha zote anachukua Rostam Aziz sasa hivyo viti watanunua kwa kutumia Mawe!!!
Poleni sana siyo lazima msome Tanzania karibuni sana upande mwingine wa dunia mje kusoma kwa starehe na raha!!!

Watanzania tumezidi upole, mtu unalipia huduma harafu unauziwa huduma duni kuliko ulicholipia na unakubali bila malalamiko au hata malalamiko kidogo tu. Mke wangu anasoma CBE na yeye analalamika tatizo hilohilo kwamba akichelewa kufika chuoni hawezi kupata kiti, hawa wanafunzi hawajawahi hata kugoma kushinikiza chuo kuweka miundombinu inayoendana na wanafunzi waliodahiliwa, na hiki ndicho kilele cha uzembe na upole huu!
Tunawachagua wanasiasa kwa ahadi kedekede na wala wasipozitimiza hatuwawajibishi ipasavyo.... SHAME on you fellow Tanzanian for being so feeble!