wisdom mapambano
Senior Member
- Jul 17, 2018
- 138
- 192
Mwanadamu unaposhiba,
usiwasahau wenye njaa.
Mwanadamu unapofanya sherehe,
usiwasahau wale walio katika matanga.
Mwanadamu unapokalia kiti cha mamlaka,
usiwasahau wale wanyonge waliopo nje ya boma.
Mwanadamu, punguza kiburi juu ya nguvu unayodhani unayo.
Jiulize: Mungu wa mbinguni ana wingi wa nyota zisizohesabika,
lakini hata hivyo huwakumbuka hata wale wanaompinga.
Na wewe ni nani?
Ulitoka tu katika tumbo la mama yako,
na hakika mauti ni kivuli chako,
hutoweza kukiepuka.
Ee wewe mfalme uliye kwenye kiti cha mamlaka,
usiwatende vibaya hawa punda katika himaya yako.
Funzo
Upendo na haki kama tunu za msingi za dhahabu zimekufa kutokana na ubinafsi wa mwanadamu. Basi ieleweke kwa kuwa Ulimwengu huu na vitu vyote viliyomo Vimeumbwa na Mungu na katika mambo yote hayo huanzia katika Ulimwengu wa Roho .
Hivyo niwatie moyo wote waliovyunjika moyo kwa Kuwa mabadiko au ukombozi huwa unakuja japo unachelewa mfano Baada ya Adamu kuanguka kama mwandamu wa kwanza ilipelekea Laana na mateso kwa mwanadamu, mpaka pale ukombozi ulipokuja kupitia Yesu kristu baada ya miaka 4000 Pia hata wana wa Israeli walikuwa Utumwani nchini Misri iliwachukual zaidi ya miaka 430 kukombolewa na Mungu.
Kupigania haki ni mchakato ambao huhitaji gharama kubwa sana kuzilipia refers Harakati za kuondoa ukoloni, Harakati hata za watu weusi nchini Marekani, n.k
Kiburi, Ubinafsi,Mauji, dhuluma, chuki, Majivuno haya ni matokeo ya Roho hio Roho iliyoasi kwa hakika hupiga sana ufahamu wa mwandamu na mtu huyo mikono yake hukimbilia katika maovu. Katika Taifa hilo mfano wa Giningi ambalo hufanya maagano ya moto uwakao siku zake za uharibifu zinahasabika.
Roho za wapendwa wote zipumzike kwa amani na wino wao uandikwe kwa maandishi ya dhahabu maaana watu hawa walitamka tu haki na hata kama ni Jinai au Madai je Malipo Yao ni kifo??🤔🥹. Ikiwa najua ya kuwa mwandamu ni nafsi tu na sio Mwili kama anavyoonekana ninatumaini la kukutana tena na wapendwa wangu nao maana kuna uzima wa milele.
Kifo wewe ni dhaifu kamwe Maadui wasikutumie kutitisha sisi tubaki katika minyororo hii,hujawahi kuizima sauti ya Haki katika Uso huu wa Dunia.
Sisi tutabeba watoto wetu na punda wetu tutakuwa mstari wa mbele kuidai Haki yetu ni Haki Yetu tunastahili na Tunaitaka
🇹🇿🙏🏾💯.