Sir Khan
JF-Expert Member
- Jul 28, 2018
- 5,361
- 9,987
Kwa muda mrefu sijapost mada hapa JF, lakini baada ya kuona upotoshaji wa peno hasegawa kuhusu kijiji cha Itumbi imenibidi kuleta mada hii.
Nimekaa kijiji cha Itumbi kwa nyakati tofauti kuanzia 2019 hadi muda huu nipo Itumbi kwa shughuli za madini. Kwahiyo ninachoandika hapa sio simulizi au stori za vijiweni.
1. Peno anadai watu wanakufa kwa kunywa maji yenye metali aina ya zebaki(mercury). Madai haya sio ya kweli kwasabu maji yanayotumika kunywa na kupikia yanauzwa na watu wa baiskeli na guta,ambao wanayachota kwenye chemichemi zinazopatika sehemu inayoitwa Guduliki a.k.a jeshini. Pia kuna watu wana visima vyao wanauza maji.
Maji yanayotoka migodini hayatumiki sana kunywa wala kupikia,pia hayana mercury kwasababu mercury haitumiki ndani ya migodi bali inatumika kukamata dhahabu baada ya mchanga wenye dhahabu kusagwa na kuoshwa huko makarashani. Baada ya hapo maji yanakuwa machafu huwezi kuyanywa, kupikia au kuoga labda uwe mgonjwa wa akili.
Naendelea.
Pia soma Waziri wa Maji, Jumaa Aweso fika wilaya ya Chunya, kata ya Makongorosi, kijiji cha Itumbi, wananchi wanakunywa maji yenye sumu ya Mercury