MwanaCCM aonekana juu ya jukwaa la CHADEMA

ina maana chadema kila mtu anapokelewa?
_hivi leo akisema aje chenge mtashangilia?

Chenge ni binadamu kama wengine akitubu dhambi zake na kuwa tayari kuwatumikia watanzania bila kuwaibia CDM itampokea.
 
Kila aombaye msamaha na kutubu dhambi zake atasamehewa na kufanywa mwana wa Mungu
 
nimepata jibu nililo hitaji.ila jamaa ana roho ngumu?
 
Huyo bwana ndiye mwenyekiti wa mtaa Madale aliyechaguliwa Jana doctor slaa alikuwa hapa Tegeta anazungumzia mgogoro wa eneo la magarage huyo bwana nikiongozi wa umoja wa watu wenye garage.
Doctor alivyo waita wenyeviti wapya na yeye alikuwepo akakaribishwa kwenye jukwaa kuungana na wenzake wa Chadema kwa sababu doctor alisema hapa sasa Ana Serikali
 
Kuna uhuni unaofanywa na viongozi wa Manispaa ya Kinondoni kuhusu ardhi katika kitongoji kile sasa wenyeviti wa mtaa wa CCM na CDM ndani ya eneo lile wameungana kupigania haki yao. Yule Mwenyekiti wa mtaa wa CCM hakuhama chama bali matatizo yao yamewaunganisha. Ni jambo la kupongezwa na si kubezwa watu wanapoweka kando tofauti zao za kisiasa na kushirikiana katika kupigania haki za wananchi wao
 
Nakubaliana na maoni yako,kama tungeweka tofauti zetu pembeni tukaungana adui angeshalegea siku nyingi maana utengano wetu ndo unawapa nguvu na tukio hilo linawaweka ktk wakati mgumu sana tufuatilie tuone kama huyo kiongozi hatawekewa mizengwe na chama chake.
 
Kuna uhuni unaofanywa na viongozi wa Manispaa ya Kinondoni kuhusu ardhi katika kitongoji kile sasa wenyeviti wa mtaa wa CCM na CDM ndani ya eneo lile wameungana kupigania haki yao. Yule Mwenyekiti wa mtaa wa CCM hakuhama chama bali matatizo yao yamewaunganisha. Ni jambo la kupongezwa na si kubezwa watu wanapoweka kando tofauti zao za kisiasa na kushirikiana katika kupigania haki za wananchi wao

Cha ajabu ni kipi? Mbona hata bungeni kwenye issue tata wabunge wote huwa kitu kimoja.
 
Sidhani kama chama chake kilifurahishwa na hatua ya mwenyekiti huyu wa mtaa wa madare
 
Nafurahi sana ninapoona wanasiasa wanaweka tofauti zao za kiitikadi pembeni nakupigania maslahi ya Wananchi... hongereni sana japo kwa jamaa wa gamba nahisi wanaweza mweka kutikavu
 
Back
Top Bottom