Mwalimu usikate tamaa

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
4,102
4,227
SHUGHULI MUHIMU ZA ELIMU.
Na Mwl.Victor Mlaki.

Katika jamii changamani pamoja n maendeleo ya viwanda elimu ina umuhimu mkubwa sana, Wanafalsafa wa vipindi vyote vilivyotangulia walionesha namna gani waliuona umuhimu wa elimu. Miongoni mwa shughuli muhimu za elimu ni:

*1.kukamilisha mchakato wa elimu jamii*Familia zimekuwa zikiwafunza watoto elimu jamii lakini familia za kileo zimekuwa zikiacha mambo mengi kuwapita watoto na hivyo shule na taasisi nyingine kuwa na jukumu la kukamilisha yale yaliyoachwa na familia.

*2.Kueneza urithi wa jamii(amali)*Jamii nyingi zinaendelea kutokana na kueneza amali za jamii kwa vizazi vyake"to transmit central heritage"Utamaduni umekuwa ukirithishwa na kusambazwa kupitia elimu, imani ujuzi,sanaa,falsafa,fasihi,dini,muziki,sayansi na teknolojia kama vipengele vya utamaduni ambao ni amali na mali ya jamii vimekuwa vikirithishwa na Susanna za kupitia elimu.

*3.Kuunda utu wa Mtu*"formation of social personality"sharti wanajimii wawe na utu unaoukiliwa na utamaduni.Elimu kila mahali imekuwa na jukumu la kuunda utu wa wanajamii.

*4.Kubadilisha tabia*Elimu ina jukumu la kuhakikisha inalinda tabia zinazohitajika katika jamii na kuzuia zile zisizohitajika katika jamii husika.

*5.Kuwaandaa wanajamii kufanya shughuli mbalimbali"occupational placement"*Waalimu wanapaswa kuhakiksha elimu wanayoitoa inawaandaa vijana kuja kushika nafasi mabalimbali katika jamii na kuwa wazalishaji(nguvu kazi ya jamii).

*6.Kulinda na kuweka hadhi katika jamii*
Katika jamii ya kileo yenye sifa ya matabaka"stratification"tumekuwa tukidhuhudia mambo yafuatayo:

(a)tathimini ya hadhi ya Mtu imekuwa aghalabu ikiangaliwa kulingana na aina ya elimu aliyoipata.

(b)miongoni mwa vigezo vingi vya kuangalia hadhi ya mtu mfano shughuli aifanyayo, kipato chake na mtindo wa maisha kwa kiasi ni zao la kiwango cha elimu aliyonayo.

*.7.Kuhamasisha ushindani*Pamoja na kutoa maarifa juu ya kushirikiana na umuhimu wa kushirikiana kupitia elimu ya Uraia na Uzalendo lakini bado msisitizo wa elimu upo katika ushindani binafsi.

*8.Kufundisha ujuzi unaohitajika kulingana na hali ya Uchumi. Peter Worsley "Uhusiano kati ya elimu na uchumi ni wa moja kwa moja" Elimu inapaswa ikidhi mahitaji ya kiuchumi na ya kijamii ya jamii husika.

*9.Kuhamasisha ushiriki wa wanajamii kidemokrasia*Idadi ya wasomi inaweza kuwa sababu ya kuruhudu ushiriki hai wa wanajamii kidemokrasia na inaeleweka usomi ni zao la elimu.

*10.Kuunganisha wanajamii*Elimu ina jukumu la kuiunganisha jamii kwa kurithisha na kusambaza amali zinazounganisha sehemu mbalimbali za jamii.

*My take* Tusikate tamaa Waalimu majukumu hayo tukiyatekeleza kikamilifu jamii itatulipa, kila jambo lina wakati wake tuendelee kuwa na imani tukiamini tunachokifanya ni mbegu na ili mbegu iote lazima pawepo na suala la kitambo kupita(subira).

Tupande mbegu njema tutavuna kwa wakati wake.
Kuna siri kubwa sana kwenye mbegu nakumbuka kwenye somo la Kilimo"Agricultural sciences"nilifundishwa kuwa mbegu ina

1.Wakati
2.Aina ya mazao.
3.Kiwango cha mazao n.k.
 
Back
Top Bottom