Mwalimu Nyerere pia alikuwa na vyeti vyenye majina tofauti

shige2

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
8,106
3,967
Wana bodi hii si uzushi wala UONGO. Tanzania tumekuwa na mtindo wa kuwa na majina tofauti katika vyeti vyetu kwa muda mrefu katika historia ya nchi yetu.Watu wakibadili badili kwa sababu hatuna mfumo wa VITAMBULISHO!

Mfano mzuri tunaupata kwa baba wa taifa Mwalimu Nyerere. Mwalimu alitumia MAJINA mawili TOFAUTI. Akiwa katika shule ya MSINGI Mwisenge huko Musoma alitumia jina TOFAUTI mpaka alipomaliza shule ya Msingi.

Kati ya Mwaka 1942 na 1943 Mwalimu akiwa na UMRI wa MIAKA 20 akiwa KIDATO cha KWANZA shule ya Tabora Government School ambayo kwa sasa ni Tabora boys AKABADILISHA jina na KUONGEZA jina LINGINE. Na hii ni vizuri MNIELEWE alifanya hivi kwa NIA NJEMA kabisa.
kama jinsi wengine tunaodai walikuwa na nia MBAYA na kumbe SIYO.

Hivi ni kusema MAJINA ya vyeti vya Mwalimu yalikuwa TOFAUTI.
S/Msingi jina lingine na
SEKONDARI hadi chuo kikuu AKAONGEZA jina lingine.

Na hivyo akawa na VYETI VILIVYOKUWA na MAJINA YALIYOTOFAUTIANA japo YALIUNGWAUNGWA. Japokuwa kwa nia njema tu.
Mwalimu Nyerere HATUKUMUULIZA kwa nini VYETI VYAKO viko TOFAUTI?

. Nini nataka kusema. Vyeti vya KUZALIWA nchini Tanzania kwetu VIMEANZA kutolewa juzi juzi tu na BADO zoezi hili halijafika mahali ambapo KILA Mtanzania atajulikana kwa jina lake HALISI.

Mpaka sasa HATUNA VITAMBULISHO vya KITAIFA. Tutabaki kulaumiana mara huyu mara nini.
Jambo linalohitajika ni vitambulisho vya KITAIFA vitolewe hapo ndo kila mtu atafahamika jina lake halisi ni nani.
Si tu katika mambo ya masomo na vyeti bali pia katika USALAMA wa taifa letu!

Chanzo: DACB-Dictionary of African Christian Biography/Catholic
 
Mkuu

Kama unajaribu kufananisha zama utakuwa ume-ba...potea njia kidogo, kama nakumbuka vizuri historia, Mwl JK aliongeza jina baada ya ubatizo na si kuwa alibadili jina kabisaaa, kwa mfano; Kambarage Nyerere, baada ya ubatizo akawa Julius Kambarage Nyerere.

Ila DAB kuwa PCM, hapa hata hiyo database inge-collapse tu.:cool:
 
Ahsante mkuu.
 
Tatizo si kubadili jina.

Kubadili jina mbona mpaka mahakamani kunakubalika?

Kambarage Nyerere alizaliwa katika dini za kiasili na kuja kuukubali Ukatoliki baadaye. Alipobatizwa kikatoliki ukubwani akapewa jina la Julius. Hilo limeandikwa. Kasome "Nyerere :The Early Years" cha Dr. Thomas Molony utaona historia yote imeandikwa. Watiama wanajua.

Tatizo ni kufanya jinai ya kubadili jina ili uchukue jina la mtu mwingine kwa nia ya kusoma au kupata faida nyingine.

Nyerere alifanya jinai hiyo?
 
Tatizo si kubadili jina.

Kubadili jina mbona mpaka mahakamani kunakubalika?

Kambarage Nyerere alizaliwa katika dini za kiasili na kuja kuukubali Ukatoliki baadaye. Alipobatizwa kikatoliki ukubwani akapewa jina la Julius. Hilo limeandikwa. Kasome "Nyerere :The Early years" cha Dr. Thomas Molony utaona historia yote imeandikwa. Watiama wanajua.

Tatizo ni kufanya jinai ya kubadili jina ili uchukue jina la mtu mwingine kwa nia ya kusoma au kupata faida nyingine.

Nyerere alifanya jinai hiyo?
Mkuu, kumbuka hapa ni VYETI viwili vyenye majina tofauti. Hilo ndo jambo JINA
 
Tatizo si kubadili jina.

Kubadili jina mbona mpaka mahakamani kunakubalika?

Kambarage Nyerere alizaliwa katika dini za kiasili na kuja kuukubali Ukatoliki baadaye. Alipobatizwa kikatoliki ukubwani akapewa jina la Julius. Hilo limeandikwa. Kasome "Nyerere :The Early years" cha Dr. Thomas Molony utaona historia yote imeandikwa. Watiama wanajua.

Tatizo ni kufanya jinai ya kubadili jina ili uchukue jina la mtu mwingine kwa nia ya kusoma au kupata faida nyingine.

Nyerere alifanya jinai hiyo?
Ukisema hivyo bssi huenda naye huyo mnayemsema basi naye ALIBATIZWA jina JIPYA!
 
Lowassa alisema kipaumbele chake ni elimu, elimu, elimu. JK alisema uvccm uwezo wao wa kujenga hoja ni wa kiwango cha chini sana...waende shule...sikuwaelewa hawa watu, sasa naanza kuelewa.

Ulikuwa na hoja nzuri sana ila uandishi ni wa hovyo kabisa as if shule yako ni ya darasa la pili...!! Lakini kibaya zaidi ni kuandika andiko refu bila hoja ya msingi.

ANDIKO LAKO LILITEGEMEWA LIBAINISHE HAYO MAJINA YA AWALI NA YALIYOKUJA BAADAYE...!!

Kwa wale waliosoma zamani kabla ya miaka ya 2000, ilikuwa kumaliza darasa la saba ukashindwa kuchaguliwa then ukaenda kurudia shule nyingine kwa jina lingine na ukafaulu na kuendelea na sekondari. Kabla ya jufika kiadato chaa pili angeweza kubadili jina lake kwa kuapa mahakamani...!!

ISSUE YA BASHITE SIYO KUTUMIA JINA LA MTU BALI NI KUTUMIA CHETI CHA MTU MWINGINE...!! HAYO NI MAMBO MAWILI TOFAUTI...!

Tafakari...!!
 
Back
Top Bottom