Ninaomba kwanza niseme wazi sina nia ya kumchongea Mzee wangu Pascally Mayega kwa Rais wetu mpendwa, wala sina nia ya kuligombanisha gazeti pendwa la Jamhuri na Rais wetu ambaye siku za nyuma aliwai kulisfia Gazeti ili.
ila kupitia gazeti la Jamhuri la tarehe 25,mwezi huu ukurasa wa kumi na tano miwandishi niliyemtaja hapo juu aliandika makala yenye kichwa cha habar NDUGU RAIS,UPANGA UNA MAKALI KUWILI
kupitia makala hiyo aliandika hoja nzito na nzuri uitimishwaji wa makala hiyo haukuwa mzuri na haukumtendea haki Raisi wa Tanzania kwani uliambatana na TUSI zito ambalo limenifanya niandike jambo ili ninanukuuuu tusi ilo
"Hatumshangai Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kwamba pamoja na kwamba ndiye Raisi mwenye umri mdogo zaidi bado anaonekana ndiye Rais anayeongoza kwa busara zaidi kuliko hata wanao onekana kumzidi umri.Hii yote si kwamba Uhuru hana ushamba urais wala hana ushamba wa Ikulu. Amezaliwa ikulu amekulia Ikulu.
Amekuwa akiyaona madaraka makubwa ya urais aliyokuwa nayo baba yake Rais Jomo Kenyatta shida ni kwetu sisi hatuna historia ya kukulia nyumbani kwa mwenyekiti. Kwetu mpaka tunaingia Ikulu ndiyo tunapata anwani. Ukiingia Ikulu lazima utakuwa mshamba. Wengi huzuzuka baada ya kutambua kuwa wamebbeba mamlaka makubwa ambayo mwanzo hawakuyafahamu"
mwisho wa kunukuuu tusi zito, sina nia au lengo la kumchochea moto ili mzee wetu awekwe korokoloni ila nina nia ya kutaka kuheshimika kwa Uraisi wa Rais wetu hata kama ametokea matopeni tuheshimu Utaasisi wa Urais huo.
Nitoe rai kwa mwariri wa jamhuri ni mhm kuhariri makala za namna hii kwani kwani sisi vijana tunaitaji kujifunza mambo mengi kutoka kwa wazee hawa ila kwa matusi haya tunaomba wabakie nayo vifuani mwao na wafe navyo ila wasivitoe.
kwa hatua zitakazochukuliwa kwa huyu mzee kutoka serikalini baada ya Bandiko ili mimi kulifikisha hapa nipo tayari kubeba lawama. kwa kuamsha walio lala.
Sent using
Jamii Forums mobile app