Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,599
- 6,669
Ludewa, Njombe
Jeshi la POLISI wilayani Ludewa Mkoani Njombe linamshikiria Abutte Fungo(40) ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi Kimelembe kwa tuhuma za kuwabaka wanafunzi wake huku akiwadharirisha kwa kuwapiga picha sehemu za siri na matiti kwa kutumia simu ya mkononi.
Wakizungumza Leo watoto hao kwenye umri kati ya mpaka 12 na 13 majina na picha tunazo wamesema kabla na baada ya kubakwa walitishiwa kuchapwa viboko, na kutishiwa kuuawa kama wangetoa taarifa kwa wazazi au mahali popote.
Kuonesha ukatiri, mwalimu huyo alimbaka mtoto mmoja Mara nane na kumlazimisha kumeza vidonge vya majira bila maji kila siku aliyofanya kitendo ili kuzuia asipate mimba.
MWALIMU alifanya vitendo hivi kati ya Oktoba na Disemba 2015 na January mwaka huu. WATOTO wanne kati ya 12 waliofika Polisi na kufanikiwa kukutana na waandishi walisema mtuhumiwa alikuwa akiwalipa pesa kati ya sh 500 mpaka 1,000 na kuongeza kuwa kila mwaka mwalimu amekuwa na tabia ya kuwabaka watoto wa darasa la 7.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Kamishna Pudenciana Protas amethibitisha kukamatwa kwa mwalimu huyo na kwamba atafikishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa.
Sosi: Mimi mwenyewe