Mwalimu Ezekia Oluochi umewageika wanao kulipa?

Mwalimu Ezekia Oluochi umewageika wanao kulipa?

NJALI

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2014
Posts
1,534
Reaction score
1,091
Mimi ni mwalimu, idara ya sekondari, tangu sijaajiriwa nilikuwa sijaona lolote la maana wanalofanya chama cha walimu.

Hawa watu licha ya kujitarisha kupitia michango yetu kwa kukata agency fee 2% ya basic salary.Sasa wamelewa na hiyo pesa hadi wamesahau ni nani amewaajiri vigogo hawa wa CWT.

Kuna mambo walimu hawatendewi haki na mwajiri wao lakini vigogo hawa wa CWT hawatoi matamko, mfano:

1.Kwa mjibu wa mkataba wa walimu wa serikali, kila mwezi wa saba kutakuwa na annual salary increment, cha kushangaza haki hii imeporwa na kuzimwa, chama cha walimu hawajatoa tamko kuhusu lini walimu wataongezewa

2.Walimu kulazimishwa kukesha kwenye mwenge na mwaajiri sengerema, sikuona Oluoch akitoa tamko wala Mikoba.

3.Walimu wa kawaida kutokupewa posho ya mazingira magumu badala yake wakuu wa shule ndio wamepewa japo sijathibitisha hilo kwa macho, niite tetesi.


Jana nilimtazama bwana Ezekia Oluoch akipongeza walimu wakuu waliozidisha wanafunzi wawajibishwe, akiongea kwa uchungu huku povu likimtoka alikazia kuisapoti serikali kwa hilo.

Sasa Oluoch Mbona hayo mambo matatu hapo juu hujayazungumzia ilihali sisi walimu ndio waajiri wako?Au alieshiba hamjali mwenye njaa?
 
Mimi ni Mwalimu, Idara ya sekondari, tangu sijaajiriwa nilikuwa sijaona lolote la maana wanalofanya CHAMA Cha Walimu.

Hawa watu licha ya kujitarisha kupitia michango yetu kwa kukata Agency Fee 2% ya basic salary.Sasa wamelewa na hiyo pesa hadi wamesahau ni nani amewaajiri Vigogo Hawa WA CWT.

kuna mambo Walimu hawatendewi haki na mwajiri wao lakini Vigogo Hawa WA CWT hawatoi matamko, Mfano:

1.Kwa mjibu WA mkataba WA Walimu WA Serikali, Kila Mwezi WA saba kutakuwa NA Annual Salary Increment, cha kushangaza haki Hii imeporwa na kuzimwa, CHAMA cha Walimu hawajatoa tamko kuhusu lini Walimu wataongezewa

2.Walimu kulazimishwa kukesha kwenye Mwenge na Mwaajiri Sengerema, sikuona Oluoch akitoa tamko wala Mikoba.

3.Walimu wa kawaida kutokupewa posho ya mazingira Magumu Badala yake Wakuu WA SHULE ndio wamepewa Japo sijathibitisha hilo kwa macho, niite tetesi.


Jana nilimtazama Bwana Ezekia Oluoch akipongeza Walimu Wakuu waliozidisha wanafunzi wawajibishwe, akiongea kwa uchungu huku povu likimtoka alikazia kuisapoti Serikali kwa hilo.

Sasa Oluoch mbona hayo mambo matatu Hapo juu hujayazungumzia ilihali sisi Walimu ndio waajiri wako?Au alieshiba hamjali mwenye NJAA?
Sina la kusema, zaidi ya kusoma na kunyamaa kimya
 
WALIMU tuamke tusiwe wanyonge Kuna masters kibao za Walimu zinafia vijijini, anaogopa akisema Ukweli atatumbuliwa, bora kufa umekaa kuliko kuishi umepiga magoti. Kuna wanafunzi tumewafundisha soon akienda CCP kuruka kichura anarudi anamshahara mkubwa kuliko Mwalimu wake aliemfundisha
 
Nimewahi kuwambia walimu wenzangu kuwa adui no moja wa maisha mabovu ya walimu ni cwt,jiulize hizo elfu ishirini wanazochukua kila mwezi unafaidikaje nazi zaidi ya t shirt ya elfu tano,

walimu tutatafuta sana mchawi lakini ukweli ni kuwa ni bora mchango wangu uende hata ccm kuliko kwa hao wasiliti wakubwa wanafiki,mungu atawalipa tu hiyo michango ya jasho la damu mnyoinyonya toka kwa walimu,hakika nawambieni
 
kwa maana nyingine mnasapoti walimu kuwaibia serikali afadhali ungeanzisha mada ukazungumzia udhaifu wa chama cha walimu kushugurikia madai yenu na sio kusapoti wizi
 
Nashauri walimu waanzishe chama chao kipya na kuachana na hao akina Oluochi maana hakiwasaidii lolote badala yake kinazidi kutunisha vitambi vya hao akina OLUOCHI na wenzake! Shame on CWT!
 
Kama kero za cwt zimeshasemwa sn lkn hakuna hatua yoyote inayochuliwa,labda tuwalaani kwa kuandamana tukiwa hatujavaa nguo pengine itasaidia
 
Hiyo namba 3 sio posho ya mazingira magumu..ni posho ya madaraka anayopewa mkuu wa shule mwenye kuanzia shahada,mwalimu mkuu(msingi) mwenye kuanzia diploma,wakuu wa vyuo na maafisa elimu kata
 
CWT ni laana tu walimu kile chama kinaogopa kutoa tamko maana wanajua mauchafu yao yataanikwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom