Mwalimu aliyekufa Aendelea Kulipwa Mshahara! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwalimu aliyekufa Aendelea Kulipwa Mshahara!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Junius, Aug 20, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 133
  Na Suleiman Abeid, Shinyanga

  HALMASHAURI ya Manispaa ya Shinyanga imekumbwa na kashfa ya ufisadi baada ya kudaiwa kutoa mkopo wa sh. milioni saba benki kwa kughushi nyaraka na kumlipa mshahara mwalimu aliyefariki dunia tangu Januari mwaka huu.

  Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili , ulibaini kuwa Halmashauri hiyo iliidhinisha mkopo huo katika Tawi la Benki la NBC Shinyanga kwenda kwa marehemu Annastazia Shija aliyekuwa akifundisha Shule ya Msingi Town.

  Pia uchunguzi huo umebaini kwamba mishahara ya mwalimu huyo iliendelea kutolewa hadi Juni mwaka huu. Mchezo uliofanyika ni wa kughushi nyaraka mbalimbali zilizowezesha kutolewa kwa mkopo huo.

  Inadaiwa kuwa udanganyifu huo ulifanywa na baadhi ya maofisa wa Manispaa ya Shinyanga kwa kushirikiana na mtu asiyefahamika ambao
  walionesha kuwa mwalimu Shija alikuwa hai na kuwa na uhalali wa kupata mkopo huo.

  Marehemu Shija wakati wa uhai wake alikuwa na akaunti katika Tawi la NMB Manonga Shinyanga ambapo ndio alikuwa akipokelea mshahara wake.

  Pia, ilibainika mtu ambaye hakufahamika alihamisha akaunti hiyo na kuipeleka katika Tawi la NBC Shinyanga ili kufanikisha njama za kukopa kiasi hicho cha fedha.

  Mmoja wa watoto wa marehemu aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina, alisema udanganyifu huo uligunduliwa na mmoja wa watumishi wa manispaa hiyo ambaye aliwapelekea 'Salary slip'(stakabadhi ya mshahara) ya Mei mwaka huu ikionesha kuwa marehemu Shija alikuwa akiendelea kupokea mshahara.

  "Kuna mtu mmoja alituletea bahasha ikiwa na 'Salary slip' ndani, baba alipoiangalia alishangaa sana, hivyo alichukua hatua ya kutoa taarifa kwa mkurugenzi ili kuweza kubaini ni vipi mishahara ya mama iliendelea kuletwa na huku ikionesha alipata mkopo wa shilingi milioni saba," alieleza mtoto huyo.

  Aliendelea kusema, mara baada ya kubainika kwa njama hizo na suala hilo kufikishwa
  Polisi, waliitwa ili kwenda kutambua picha iliyobandikwa katika fomu za mkopo ambapo
  ilikuwa ni ya mtu mwingine ingawa majina na maelezo mengine yote yalikuwa ya marehemu.

  "Kabla ya mama kufariki, nilikaa naye na akanieleza kuwa hakuwa adaiwi na mtu yeyote
  yule na wala hana mkopo wowote wa benki na hata katika chama chochote cha akiba
  na mikopo (SACCOS), kwa kweli tumesikitishwa na kitendo hiki, tunasubiri taarifa za
  Polisi ili tujue mtu aliyefanya mchezo huo," alieleza.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Bi. Jane Mutagurwa, alikiri kuwepo tukio hilo la udanganyifu uliofanywa na watu ambao alidai ni wa nje ya ofisi yake.


  Kuhusu mishahara ambayo iliyoendelea kutumwa, alisema ofisi yake imekuwa ikiirejesha Hazina kila mwezi na kuwataka waandishi kuwasiliana na hazina iwapo watakuwa na wasiwasi wowote kuhusu mishahara hiyo.

  "Ni kweli hata mishahara inaendelea kuletwa, lakini hili si tatizo la ofisi yangu ni
  tatizo la watu wa Hazina, kila inapotumwa tunawarejeshea na kuwaeleza kuwa mwalimu
  huyo aliishafariki dunia lakini tunashangaa imekuwa ikitumwa mpaka sasa," alieleza Bi. Mutagurwa.

  Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Bw. Daudi Siasi, amekiri kuwepo tukio hilo na kwamba polisi hivi sasa inafanya uchunguzi ili kuwabaini watu waliohusika na kitendo hicho ikiwa ni pamoja na kumpata mtu aliyebandika picha zake katika fomu za mkopo.

  SOURCE: MAJIRA
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 133
  Du, Kwa Mungu kuna kazi kesho!
   
 3. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #3
  Aug 20, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,282
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  hizi zipo sana mzee!
  nchi yetu ndo inavyokwenda
   
 4. M

  Msindima JF-Expert Member

  #4
  Aug 21, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Makubwa haya nchi hii kwa kweli inahitaji msaada wa Mungu!
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Aug 21, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  balaa tupu
   
Loading...