Mwalimu akatwa mkono kisa wivu wa kimapenzi

digba sowey

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
4,860
2,000
Mwalimu wa Shule ya Sekondari Kiranyi Arusha Veronica Kidemi amesema Mume wake amemkata kiganja chake na kukitenganisha kabisa na mkono kutokana na wivu wa mapenzi.

“Mume wangu amekua akinituhumu mara nyingi kwamba anasikia nina chepuka kwenye mapenzi lakini nilishamwambia anipe ushahidi na sio tu kusema anasikia na sio kila Mtu anapenda ndoa yake kuwa na amani, Yeye anafanya kazi Dar... juzi aliniambia nikachukue kilichochangu nifungashe”

“Juzi Ijumaa niliporudi nyumbani akawa amerudi bila taarifa, akanikimbilia na kuanza kunishambulia niliishiwa mpaka pozi na akatenganisha kiganja changu na mkono... alinikatakata kama anafyeka, alikua hataki hata niende kwa Ndugu yangu”

Source Millard ago
FB_IMG_1601477629106.jpg
 

Kohinoor

JF-Expert Member
May 28, 2020
241
250
Ungekuwa Mara mikelele kibao lakini chuga fresh mto was mbu fresh acheni kukariri sku hiz matukio ya namna hiii yako kila sehem Tena mara yamepoa Mana sehemu nyingine mmh matukio ya ukatili wa namna hiii ni makubwa mno
 

Sir_Mimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2013
6,710
2,000
Kuna kisa nilikisoma humu jana na kipo kingine miaka minne kama siyo mitano nyuma nilikisoma humu humu ila hivyo viwili kimoja ni mume Mwalimu anateswa na kusimangwa na mkewe (cha jana) na kingine jamaa aliuwa mke mwalimu na hawara kisha akatembea.

Hata huyu nachelea kusema alikuwa siyo msaliti,haiyumkiniki uambiwe tu from no where na mumeo kwamba unasaliti agano najua lazima ilitokea akamletea mumewe dharau plus majivuno sasa jamaa alipounga dots akaona huu ni ukweli akaamua aondoke nae mzima mzima,as usual anategemea kilio eti nilimwambia alete ushahidi,ulitaka apige picha mkizini???
 

Yna2

JF-Expert Member
Aug 18, 2018
22,238
2,000
Wanaume mkiwachoka wake zenu muwaache..yanini kupeana ulamavu wa ukubwani kisingizio wivu..!!??
Huu ni ukatili jamani.
 

Maili tatu

JF-Expert Member
Aug 8, 2020
423
1,000
Binadamu wengne jazba zao zinafika hadi Jupiter na hapo alitamani kumtoa nyonga yote,mapenzi mapenzi hayachezewi roho ya MTU inaweza toka mda siyo mrefu,matukio haya ni meng tu sema media imelipata hili .hatujui makosa ya wote wawili kabla ya tukio hili
 

Fall Army Worm

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
10,383
2,000
Jamanii
Huu ni zaidi ya unyama .
Kama umemchoka mtu so unamuacha tu jamani, kwani lazima umfanyie ukatili!?!
Unadhani ni unyama??!!?,Kwa haraka unaweza kutafsiri kuwa ni unyama lkn hapo ni Upendo uliopitiliza umeenda kwenye wivu,Mtu mwenye wivu na wewe(kwa wapenzi) ujue anakupenda balaaa.
 

B'REAL

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
4,056
2,000
Mkuu tunahukumu tu ushaambiwa jamaa yuko kikazi dar mama yuko Arusha jamaa alipata tarifa anagongewa...hivi unajua uchungu wa mkee bwasheeew
 

Ngishi

Senior Member
Sep 17, 2018
119
250
Ukiona mwenzio anachepuka km huwezi kuvumilia achana naye usilazimishe kupendwa ukijifanya mbishi matokeo yake mabaya ona Sasa dada wa watu kapewa kilema mbaya zaidi mwanaume anaenda kunyea debe na kibarua amekipoteza,Uhuru wa kuishi aliokuwa nao hamna Tena,watoto wanakosa mapenzi ya baba pamoja,mama yao alikuwa Hana kilema anarudi na kilema kisa baba yao mwisho wanakuwa na chuki binafsi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom