tikatika
JF-Expert Member
- May 6, 2011
- 2,330
- 4,119
Mungu aliye tupatia akili tunapaswa kumshukuru kila siku. Na leo namshukuru kwa kunipa akili za kumwelewa waziri mwakyembe.
Wakati akijibu hoja za Juma mkamia juu ya kuhudhuria kwake katika press ya Roma mkatoriki waziri amejaribu pia kutupa ripoti tunayoisubuiri ya ndugu yetu Roma na wenzake kutekwa. Akijibu hoja hizo anasema kwenda kwake ni sehem ya upelelezi ili watanzania waondokane na hizi ramli za mitandaoni na bungeni juu serikali kuhusika katika tukio hilo. Anasema yafuatayo;
Nilikwenda pale ili nijue ukweli juu ya tukio lile na kijana ameniambia vitu tofauti na ramli za humu bungeni na mitandaoni juu ya serikali kuhusika kumteka. Anasema mtu aliye mteka anamjua na anaomba upelelez ukamilike haraka. Anavyosema kijana ni tofaut kabisa na ramli zenu humu na huko nje.Anasema waliomteka walienda na bastora. Na kwa kwenda na bastora haina maana ni serikali maana bastora tunazo wengi tu. ni tofauti na majibu ya awali ya wahusika kwamba walitekwa na watu wenye bunduki. Wakimaanisha siraha nzito. Sasa tujiulize haya kidogo;
Je kuna haja gani ya kusubiri upelelezi wakati waziri kaishatoa mwanga na kaishatoa hukumu kwamba serikali haihusiki??
Kingine yeye ni sehem ya timu ya upelelezi?
Je alitumwa atoe hayo majibu??
Kingine mbona serikali iko mbio sana kujitoa katika kuhusika kuna nini.
Nije kwenu wananchi wenzangu hivi tulitegemea serikali kukubali kuhusika kwake katika tukio lolote baya kwamba imehusika. Hebu nipeni mfano mmoja unaofanana na haya matukio yanayoshabihiana na kutoa uhai wa raia na serikali ikakiiri kuhusika.
Niende kwa Roma ; ndugu Roma ni kweli mimi siwez kukusaidia lakn kaa ukijua usitegemee serikali ijuchunguze ikuletee mabaya yake . Kamwe haitatokea. Nikukumbushe mwangosi aliuwawa peupe na katikati ya askari wengi lakn serikali ilikana kwamba haihusiki bali ni kiherehere cha huyo askari mmoja japo hata sura hatukuwahi kuonyeshwa. Yule aliye watuma akapandishwa cheo. Wale askari wakabaki kama kikosi kinacho jitegemea na hakijatoka serikalin kwa amri ya afisa wa police ili awajibike. Askari police wenzake na yule aliye ua mpaka kesho wanaendelea na kazi zao. Sasa Uweni nyie raia muwe wanne uone kama hukumu atapewa aliyeshika kisu tu.
Sasa hofu yako Roma ilikua nini kutotwambia sisi watanzania wenzio ila ukamwona huyu waziri ndio mwokozi wako!? Jiangalie hawana rafiki hawa watu.hata waliotaka kumteka Nape hawawajui, japo mpaka kesho utaendelea kuwaona kwenye mitandao na walifanya tukio mbele ya waandishi wa habari. Lakn mpaka kesho serikali inasema haiwatambui japo kila mmoja tulimwona na pisto kiunoni achilia mbali yule aliye tishia juu. Kama wamefanya hivi kwa Nape utakua wewe??
Ombi kwa police hamna haja ya kutucheleweshea taarifa waziri kasha twambia njooni mfanye marudio. Hebu msikilize hapa.