Hadija Jumanne na Deborah Ngajilo
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amesema wananchi wampe muda wa miezi sita ili aweze kukamilisha miundo mbinu katika sekta ya reli nchini.
Dk Mwakyembe aliyasema hayo jana jijini Dar es salaam wakati akifungua mkutano wa pili wa wataalamu unaohusu Takwimu (Logistic) kwa Africa katika miundo mbinu.
Mbali na kutoa muda huo, Dk Mwakyembe amekiri kuwapo kwa tatizo la usafiri hapa nchini na kuomba washiriki katika mkutano huo kutatua matatizo yanayoikumba sekta hiyo ikiwamo matumizi ya teknolojia mpya ya usafirishaji nchini, usambazaji wa mdogo wa chakula na Sekta ya Reli.
Katika mkutano huo , Dk Mwakyembe alisema miezi sita inatosha kukamilisha ahadi ambayo aliitoa na kwamba hatua hiyo inatokana na wananchi kuhoji usafiri huo wa reli utaanza lini wakati Serikali ilitangaza usafiri huo utaanza Oktoba Mosi mwaka huu. Nipeni muda wa miezi sita ili muweze kuona sekta ya reli itakavyokua imekamilika nchini, kwa kuwa sekta ya reli ni muhimu katika maendeleo ya nchi hivyo ni vyema tukaitengeneza ndani ya miezi hiyo kupitia wataalamu wetu,alisema Dk Mwakyembe.
Tuacheni tufanye kazi na nyie endeleeni kutunga ngojera kuhusiana na usafiri wa reli lakini sisi tunajua tunachokifanya kwani niliposema usafiri wa reli unaanza mwezi Oktoba sikumaanisha utaanza Oktoba Mosi kwani hata Oktoba 15 ipo ndani ya mwezi huo huo,.
Alifafanua kwamba kwa sasa wameanza kungoa reli na kuweka yenye uzito wenye paundi 95 ambao wanashirikiana na Benki kuu katika kubadilisha usafiri wa reli katika Mkoa wa Dodoma.
Alisema lengo la mkutano huo ambao umehusisha mabingwa wa mfumo wa takwimu ni kujadili umuhimu wa usafirishaji hasa wa reli, mafunzo kwa wataalamu katika mambo ya miundo mbinu pamoja na usalama wa chakula na usafirishaji.
Alisema ili soko liweze kuendelea vizuri linahitaji wasambazaji wawe na usafiri mzuri ikiwamo wa miundo mbinu mizuri ili kuwafikia watumiaji.
Alisema mkutano huo utaongeza uzoefu kwa washiriki katika masuala ya miundo mbinu katika Afrika kwa kuwa sekta ya usafirishaji ni muhimu katika maendeleo ya uchumi dunia.
Awali Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji nchini (NIT), Mhandisi Zacharia Mganilwa alisema lengo la mkutano huo ni kujadili jinsi ya kukabiliana na maafa yanayojitokeza kipindi cha maafa ya asili na shughuli za kibinadamu ikiwemo mafuriko.
Maafa ya asili ni kama mafuriko yanapotokea sehemu ambazo miundo mbinu mibovu husababisha misaada kushindwa kufika kwa wakati hivyo kama chuo kikishirikiana na wataalamu tunaweza kutatua matatizo haya na misaada au bidhaa kufika kwa wakati,alisema Mhandisi Mganilwa.
Mhandisi huyo alisema umuhimu wa kuwa na miundo mbinu ya reli katika kusafirisha mizigo lina hitaji kuwa na wataalamu ambao watasaidia katika kuondoa kero zinazotokea.
Mkutano huo wa siku mbili umeandaliwa na Ubalozi wa Ujerumani ukishirikiana na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) ambapo zaidi ya nchi kumi kutoka nchi mbalimbali duniani zimeshiriki. Mwakyembe: Nipeni miezi Sita
Mh. Waziri Mwakyembe Tunakupa hiyo miezi Sita Fanya vitu vyako kuhusu Reli ........
Give him time!Yeye ni mtaalamu wa sheria tuu, ni lazima afanye kazi pia kwa kuzingatia ushauri wa wahandisi kuepusha maafa na Lawama! Be patient, vitu vizuri havitaki haraka za kisiasa!ni utaalamu pia unawekwa mbele
tumpe muda reli iliyopo kwa kweli imechoka
nimeona wakibadilisha tusubiri imalizike tusafiri kwa usalama na uhakika.
ikitokea ajali tutakuwa wakwanza kulaumu kwanini aliruhusu tren kutumia miundo mbinu chakavu.