Mwakyembe: Niko tayari kusulubiwa

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,710
2,226
Aweka wazi kuwa hafikirii kuteua wabunge kushika nyadhifa ndani ya wizara yake

na Datus Boniface

WIKI kadhaa tangu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe kutengua nafasi ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Paul Chizi, amesema yuko tayari kusulubiwa kwa kuchagua watu wenye sifa kushika taasisi mbalimbali zilizopo chini ya wizara hiyo.

Mwakyembe alimtimua Chizi na badala yake alimteua Kapteni Lusajo M. Lazaro, kukaimu nafasi hiyo kuanzia Juni 4, huku akiwasimamisha kazi maofisa wengine wanne wa ATCL akiwemo Kaimu Mkurugenzi wa Uhandisi, John Ringo.
Jana, wakati akizindua Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Huduma ya Meli (MSCL), Mwakyembe aliweka wazi juu ya azma yake hiyo na kusema sifa za mtu zitatumika kama kigezo cha kuongoza.
“Sifa za mtu zitaongoza taasisi mbalimbali, hata kwenye bodi za wizara watateuliwa watu wenye sifa, na nyinyi mlioteuliwa tafuteni njia yoyote ya kuiinua MSCL,” alisema.
Katika taarifa yake kwa bodi hiyo, Mwakyembe aliweka wazi kuwa hadhani wala kufikiri kuteua wabunge kushika nyadhifa zozote zile ndani ya wizara yake.
Hata hivyo, aliwaonya wajumbe na Mwenyekiti wa Bodi ya MSCL, Salim Msoma, ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara, kuhakikisha wizi, uzembe, ubadhirifu na utendaji usioridhisha unapigwa vita na kuondoka.
“Hakikisheni hesabu za kampuni zinakaguliwa kila mwaka kwa mujibu wa sheria, na kwamba maagizo ya wakaguzi yanafanyiwa kazi bila kuchelewa,” alisema.
Pia, aliitaka bodi hiyo kutangaza na kuajiri Meneja Mkuu wa kampuni na nafasi nyingine ambazo ziko wazi.
Aidha, aliiagiza kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato yatokanayo na huduma na matumizi ya kampuni.
Awali, Mwenyekiti wa bodi hiyo, Msoma alisema wako tayari kukabiliana na changamoto zozote na kuzishughulikia.
 
Back
Top Bottom