Waziri wa Uchukuzi, Dr. Mwakyembe, amethibitisha kuwa anachakachua ripoti ya Tume aliyoiunda kuchunguzz tuhma za bandari baada ya kuwaambia waandishi wa habari kwamba leo ndio amepokea baada ya kuirudisha kwa tume aliyoipokea awali ma pia amesema atahoji watu waliokataa kushirikiana na tume aliyoiunda na kuipa wiki mbili lakini ikatumia miezi miwili kwa gharama za Bandai. Sina hakika kama ana mamlaka kuunda Tume. Tundu Lissu alisema Waziri hana mamlaka kisheria kuunda tume, pale Nchimbi alipounda ya kuchunguza mauaji ya Mwangosi🙂 mmoja wa waliokuwapo kwenye Press Conf ya Mwakyembe anasema;
"Hiyo ya kupokea report mbili kwa siku tofauti ni uthibitisho tosha kuwa kumekuwa na uchakachuaji mkubwa kwenye report hiyo. Hii kuwaita watu wengine ambao hawakuhojiwa na kamati offisini kwake ili awahoji mwenyewe *si utawala bora kabisa na tafsiri yake ni witch hunting yaani kuwindana wakati biashara ikiendelea kudorora."
Tanzania Daima la jana liliandika:
Mwakyembe kuanika kiini cha hasara Bandari
na Mwandishi wetu
WAKATI Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, anakutana na watendaji
wake na waandishi wa habari, imethibitika kwamba Mamlaka ya Bandari Tanzania
(TPA) imepata hasara kubwa.
Taarifa za uhakika ndani ya TPA zimeeleza kwamba kwa kipindi cha mwezi
Septemba, 2012 mapato ya Bandari yameshuka kwa asilimia 13.3, sawa na shilingi
bilioni nane.
Mapato hayo kwa mujibu wa maofisa wa TPA yameshuka kutokana na kuzorota kwa
ufanisi bandarini uliotokana na uwezo duni wa uongozi mpya uliosimikwa na
Mwakyembe katika mazingira tata.
Ufanisi umepungua sana na sasa mwezi Septemba tumepoteza biashara kwa kiasi
kikubwa kutokana na huduma kudorora. Oktoba hasara inaweza kuwa mara mbili
kama tutaendelea kufanya siasa katika sekta nyeti ya bandari, anasema ofisa
mmoja mwandamizi bandarini.
Ofisa huyo pamoja na kumsifia Mkurugenzi mpya wa TPA, Madeni Kipande,
amesema kutokana na kutokuwa na uzoefu katika sekta ya bandari, upo uwezekano
mkubwa wa kuharibiwa sifa yake ya uadilifu na uchapa kazi.
Namfahamu Kipande si mtu mbaya na ana uwezo, lakini kwa dude kubwa kama
bandari hatoweza na hasa ikizingatiwa ameingizwa kisiasa na anapokea amri za
kisiasa badala ya kitaalamu. Hatari nyingine ni mahusiano yake ya kidugu na
uongozi wa juu wa nchi yanaweza pia kuipaka matope serikali, anasema.
Kipande ambaye alitokea serikalini, ametajwa kuwa anatokea mkoani Pwani,
pamoja na yeye mwenyewe kusema mahusiano yake na uongozi wa juu serikalini
yamemponza kukosa nafasi nyingi serikalini badala ya kuwa msaada kwake na
kwamba TPA amekwenda kibahati.
Katika kikao hicho, Dk. Mwakyembe anatarajiwa kutoa taarifa ya tume aliyoiunda
kuchunguza tuhuma mbalimbali zinazowakabili viongozi wa TPA, tume aliyoiunda na
kuipa wiki mbili kumaliza kazi, lakini ilifanya kazi kwa zaidi ya miezi miwili kwa
gharama za TPA.
Waziri Mwakyembe anaelezwa kupokea ripoti hiyo na kuichambua, kabla ya
kumshirikisha Rais Jakaya Kikwete, aliyekuwa safarini nchini Oman, alikorejea juzi
Ijumaa.
Rais Kikwete ndiye mwenye mamlaka ya uteuzi ya Mkurugenzi Mtendaji wa TPA,
Ephraem Mgawe, aliyesimamishwa.
Taarifa za ndani ya serikali zimeeleza kwamba kumekuwa na shinikizo kutoka
serikalini kutaka uongozi uliosimamishwa urudishwe kazini kwa masilahi ya taifa
kutokana na kuonekana pengo kubwa katika mfumo wa bandari.
Tayari kumekuwapo taarifa za kuwapo hofu ya kuchakachuliwa kwa ripoti hiyo na
tayari baadhi ya viongozi waliosimamishwa wanatarajiwa kuhamishiwa maeneo
mengine.
Imeelezwa kwamba tayari Dk. Mwakyembe amekwisha kuandaa nafasi SUMATRA
ambako anapanga kuwahamishia viongozi hao.
Imeripotiwa katika baadhi ya magazeti kwamba huduma nyingi zimeanza kuzorota
katika Bandari ya Dar es Salaam, na kusababisha usumbufu kwa wateja huku baadhi
ya makampuni ya meli yakihamia bandari nyingine na wanaobaki Dar es Salaam
wanahamia TICTS.
Mwakyembe aliunda tume hiyo Agosti 24, 2012 na kuipa wiki mbili lakini ilichukua
karibu miezi miwili ikiendesha shughuli zake katika hoteli moja kubwa Dar es Slaam
lakini imegubikwa na utata mkubwa kutokana na inavyoendesha shughuli zake.
Taarifa za ndani ya TPA zimeeleza kwamba uongozi mpya wa bandari kwa sasa
umeshindwa kufanya kazi kutokana na kuendelea kuwapo makundi ndani ya
mamlaka hiyo, huku baadhi ya waliochukua nafasi wakiwa hawana uwezo wala
uzoefu katika sekta husika.
Kabla ya kuunda tume hiyo, Dk. Mwakyembe aliwasimamisha kazi viongozi wote wa
TPA, akiwamo Mkurugenzi Mkuu, Ephraim Mgawe akiwatuhumu kuhujumu uchumi
na kukaidi maagizo ya Ikulu, tuhuma ambazo tume inahaha kuzichimba kila kona,
ikiwa ni pamoja na kurubuni baadhi ya watu.
Pamoja na Mgawe, wengine waliosimamishwa kazi ni naibu wakurugenzi wakuu
wawili wa TPA waliotajwa kwa jina moja moja la Mfuko na Koshuma. Pia yumo
Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Cassian Ngamilo, Meneja wa Kurasini Oil Jet,
Meneja wa KOJ na Terminal Oil Engineer, ambao hawakutajwa majina.
Mwakyembe alimteua Madeni Kipande ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Barabara
katika Wizara ya Ujenzi kukaimu nafasi ya Mgawe.
www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=41757