Mwakyembe kuwa waziri pigo kwa Lowassa

Mwakyembe kuwa waziri pigo kwa Lowassa

sikiolakufa

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2010
Posts
411
Reaction score
55
Ni dhahiri uteuzi wa Dr.(Phd) Harrison Mwakyembe kuhudumu kama waziri kamili katika serikali ya Kikwete ni pigo kwa Mbunge wa Monduli( waziri Mkuu aliyejiuzuru) Mbunge huyu alichukizwa sana kuhusishwa na sakata la mradi hewa wa uzalishaji umeme lililomg'oa katika nafasi yake ya Waziri Mkuu. Dr.(Phd) Mwakyembe alitenda haki kwa majukumu yake ya kamati ya bunge ingawa alionekana adui kwa kufichua uovu...leo hii Rais ameridhishwa na utendaji wake na uzalendo wake...pole Lowassa
 
Namshauri Lowassa not to take it personally kwa uteuzi huu.
Lakini ni wakati huu miaka sita baadaye ndo Ngeleja anaondoka mahali pale penye harufu ya madudu.
Tusisahau kuwa Ngelej na tumizizi twa ushirikiano n watuhumiw wa Richmond.
Prosecutor in,prosecuted out.
 
Ni viongozi wachache sana wenye moyo na ujasiri kama wa MR Mwakyembe
 
Wizara aliyopewa Mwakyembe ni wizara yenye changamoto nyingi; kwanza ni watendaji wakuu wa ile wizara ni mzigo, kwani wanauhusiano wa moja kwa moja na Ikulu hivyo mwakyembe itabidi athibiti hali hiyo kwasababu ndio chimbuko la majungu. Pili katika utendaji wake itabidi hasa kwenye uteuzi wa mabodi ni lazima aheshimu professionalism na sio uswahiba kama wanavyofanya waswahili. Akifanya hivyo kazi itamuwia rahisi.
 
Sidhani kama maelezo yako yana mtiririko kuleta mantiki. Na pia Mwakyembe ni sehemu ya tatizo (kwa aina yake), Lowassa aliiba, Mwakyembe akasema sehemu ya kilichoibiwa.

Tusiwe wepesi kummwagia sifa asizostahili mtu. Pia tusiwe wepesi kulaumu asivyostahili mtu. Juzi tu Filikunjombe walimwona shujaa kama walivyowahi kuwaona kina Kilango, Simbachawene, Sendeka nk lakini niambie leo hao watu wanasimama wapi?

Mwakyembe ni opportunist politician, trust me. He's also a very good academician. Each should be contextually judged.
 
Kwa kweli unaweza kutufafanulia? kwanini kuandika habari za kifitina bila source? Mwakyembe alikuwa Naibu Waziri, na Sasa Waziri kuna utofauti?

Jamani Sasa tumekuwa tunapaparuka na Hoja zisizo na source, kama ni nchi za magharibi hapo unashitakiwa na kulipa mamilioni ya Dollars... Shukuru uko Bongo
 
mtu akifanya kazi kikatiba kama vile alivyoapa mbele ya Rais watu wanamuona mbaya, wanaamua kumloga au kumpa sumu.. hivi kwanini mawaziri wanakula viapo wakati wanajua hawatatekeleza hata kimoja ambacho wanaapia pale ikulu? unakuta na lijitu lizima limeshika na bible kumbe ni jizi la kuotea mbali
 
Back
Top Bottom