Mwakyembe ashuhudia madudu Ubungo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080
mwakyembe%20mabasi(1).jpg

Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, akizungumza na waandishi habari mbele ya abiria na wahudumu wa mabasi kwenye Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam jana. Mwakyembe alifanya ziara ya kushtukiza kufuatia ripoti kuwa nauli za usafiri wa mabasi ya mikoani zimepanda maradufu kwa kile kinachodaiwa na watoa huduma ni ongezeko la abiria katika kipindi hiki ambapo wanafunzi wanarejea shuleni kutoka likizo ndefu.


Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, amefanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani, Ubungo na kuendesha operesheni ya kukamata magari yanayotoza nauli kubwa kinyume cha sheria ambayo yametozwa faini ya Sh. 250,000 kwa kila kosa.

Kadhalika, mabasi 25 yalikamatwa kwa kosa la kupandisha nauli kiholela na kutozwa faini na kuamuriwa kuwarudishia abiria wote pesa zote walizozidisha.

Dk. Mwakyembe aliwasili Ubungo majira ya saa 10:30 alfaji na kuanza kuendesha operesheni hiyo ambapo jumla ya mabasi 65 yalifanyiwa ukaguzi na baadhi ya magari yalibainika kutoza nauli kubwa kinyume na ile iliyopangwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra).

Alisema amelazimika kufanya ziara ya kushtukiza, baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi wakilalamikia kupanda kwa nauli kiholela.

Katika operesheni hiyo, Dk. Mwakyembe ametoa onyo kwa viongozi wa Sumatra kwamba kama hawezi kufanya kazi hiyo hadi wamsubiri yeye (Dk. Mwakyembe) ni bora waiachie ofisi hiyo.

Akizungumza na NIPASHE jana baada ya kufanya ukaguzi huo, Dk. Mwakyembe alisema baadhi ya mabasi yaliyokamatwa yalikutwa na makosa hadi matatu ambapo yalitozwa faini ya Sh. 750,000.

“Suala la mabasi kutoza nauli kubwa linalalamikiwa sana na wananchi, sasa kwa kweli kama Sumatra wanaona hawawezi kufanya kazi ya ukaguzi na kuchukua hatua itabidi waiachie ofisi,”alisema Dk. Mwakyembe.

Alisema ukaguzi unaofanywa na Sumatra umebaini kwamba mabasi yote ya abiria yanayokwenda masafa marefu kama kutoka Dar kwenda Mwanza yanaendeshwa na dereva mmoja jambo ambalo siyo sawa.

“Mabasi yanayokwenda mbali zaidi kama Mwanza yanatakiwa kuwa na madereva wawili, sasa katika ukaguzu huu, tumegundua mabasi mengi yanaendeshwa na dereva mmoja tu,” alisema.

Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Hemedi Kilima, alisema zoezi hilo ni endelevu, na kwamba wataangalia kwenye rekodi za Sumatra, ili kujua kama mabasi hayo yalihusika kwenye ukaguzi uliofanywa Januari mwaka huu, na endapo itathibitika kuwa yalihusika yatanyang’anywa leseni.

Hii ni mara ya pili kwa Dk. Mwakyembe kufanya ziara Ubungo baada ya kufanya hivyo mapema mwishoni mwa mwezi uliopita.




CHANZO: NIPASHE

 
Back
Top Bottom