OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,021
- 114,388
DK. Harrison Mwakyembe, Waziri
wa Katiba na Sheria, amesema
kuwa Tanzania ni bora iendelee
kutaambika na watanzania wafe
wakiwa masikini kuliko
kuendelea kunyanyaswa na
mataifa ya ulaya, Mwakyembe ambaye
hata hivyo hakuyataja
mataifa hayo lakini moja
kwa moja ilionekana
kuyagusa baadhi ya
mataifa ya Ulaya pamoja
na Serikali ya Marekani
iliyovunja uhusiano na
Serikali ya Tanzania
katika mambo yote
yanayohusu miradi ya
maendeleo
inayofadhiliwa na mfuko
wa changamoto za
millenia (MCC).
Mwakyembe ametoa kauli hiyo
wakati akizungumza na
watumishi wa wizara ya katiba
na sheria jijini hapa, ikiwa ni
mwendelezo wa ziara yake ya
kikazi kwa mkoa wa Mwanza.
Mwakyembe ambae pia ni
mbunge wa Jimbo la Kyela
mkoani Mbeya, amesema kuwa
anashangazwa na baadhi ya
watu wanaotaka kuliingiza taifa
katika mambo mabaya yasiofaa
na yalioko kinyume na maadili ya
watanzania.
Amesema mataifa hayo
yamekuwa yakionekana
kuilazimisha Tanzania kuingia
katika mambo yasiyokubalika na
watanzania wenyewe ikiwemo
suala la `shoga` kitendo
ambacho alidai ni cha hovyo.
“Ni bora tufe masikini kuliko
kuendeshwa kwa hofu, wao
wanataka watuendeshe tu, sisi
vitu kama vya shoga vinapaswa
kupingwa vibaya na haiwezekani
kabisa.
“Vitu kama vya shoga ni vya
hovyo na kama watanzania
hatukubaliani navyo, hata maadili
yetu yenyewe hayataki mambo
kama hayo,” amesema
Mwakyembe.
Machi 29 mwaka huu, Serikali ya
marekani kupitia kwa bodi ya
wakurugenzi wa MCC ilitangaza
uamuzi wa kuinyima Serikali
Dora za kimarekani Milioni 472.8
( zaidi ya Sh. Trioni 1 na bilioni
20) kutokana na marudio ya
uchaguzi wa serikali ya Zanzibar
na sheria ya makosa ya mtandao.
wa Katiba na Sheria, amesema
kuwa Tanzania ni bora iendelee
kutaambika na watanzania wafe
wakiwa masikini kuliko
kuendelea kunyanyaswa na
mataifa ya ulaya, Mwakyembe ambaye
hata hivyo hakuyataja
mataifa hayo lakini moja
kwa moja ilionekana
kuyagusa baadhi ya
mataifa ya Ulaya pamoja
na Serikali ya Marekani
iliyovunja uhusiano na
Serikali ya Tanzania
katika mambo yote
yanayohusu miradi ya
maendeleo
inayofadhiliwa na mfuko
wa changamoto za
millenia (MCC).
Mwakyembe ametoa kauli hiyo
wakati akizungumza na
watumishi wa wizara ya katiba
na sheria jijini hapa, ikiwa ni
mwendelezo wa ziara yake ya
kikazi kwa mkoa wa Mwanza.
Mwakyembe ambae pia ni
mbunge wa Jimbo la Kyela
mkoani Mbeya, amesema kuwa
anashangazwa na baadhi ya
watu wanaotaka kuliingiza taifa
katika mambo mabaya yasiofaa
na yalioko kinyume na maadili ya
watanzania.
Amesema mataifa hayo
yamekuwa yakionekana
kuilazimisha Tanzania kuingia
katika mambo yasiyokubalika na
watanzania wenyewe ikiwemo
suala la `shoga` kitendo
ambacho alidai ni cha hovyo.
“Ni bora tufe masikini kuliko
kuendeshwa kwa hofu, wao
wanataka watuendeshe tu, sisi
vitu kama vya shoga vinapaswa
kupingwa vibaya na haiwezekani
kabisa.
“Vitu kama vya shoga ni vya
hovyo na kama watanzania
hatukubaliani navyo, hata maadili
yetu yenyewe hayataki mambo
kama hayo,” amesema
Mwakyembe.
Machi 29 mwaka huu, Serikali ya
marekani kupitia kwa bodi ya
wakurugenzi wa MCC ilitangaza
uamuzi wa kuinyima Serikali
Dora za kimarekani Milioni 472.8
( zaidi ya Sh. Trioni 1 na bilioni
20) kutokana na marudio ya
uchaguzi wa serikali ya Zanzibar
na sheria ya makosa ya mtandao.